• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

TUNDURU YAZINDUA JUKWAA LA UWEKEZAJI WANAWAKE KIUCHUMI

Imewekwa : August 15th, 2017

Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imetekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan la kila Halmashauri nchini kuanzisha jukwaa la uwekezaji wanawake kiuchumi,jukwaa hili litaunganisha wanawake kutoka kada tofauti tofauti na kutoa fursa za Uchumi, Biashara,upatikanaji wa mitaji, na kupitia sheria za nchi katika masuala ya Uchumi na jinsia ya kujitegemea kiuchumi.

Akizungumza na wanajukwaa mkuu wa wilaya ya Tunduru ambaye pia alikuwa mgeni katika uzinduzi wa jukwaa hilo Mh.Juma Zuberi Homera alisema jukwaa hili litawasaidia wananwake kujikwamua kiuchumi kwa watapata sehemu ya kusemea matatizo yao yanayowakabili na changamoto mbali mbali, pia jukwaa hili litawasaidia katika kupata mikopo ya asilimia tano kutoka halmashari kwani watapata sehemu ya kuweza kukutana na kupanga mipango ya uchumi, biashara na njia za kuweza kupata mikopo na kuongeza kipato kwa kimama.

Vilevile jukwaa la uwekezaji wanawake kiuchumi wilaya litakuwa na tija kwa kina mama kwa sababu litaongeza wigo wa kuweza kupata wakufunzi wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa kuwa watakuwa na chombo cha kuwaunganisha niwaombe viongozi wa jukwaa hili mtumie nafasi zenu katika kuleta mabadiliko katika wilaya  ya Tunduru

Mh. Homera alisema kuwa "ili jukwaa hili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi linatakiwa kuwa mambo yafuatayo ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti ya wanajukwaa, kuwa ofisi maalum ambayo shughuli zote za wanawake zitakuwa zinafanyika, kuwa na ushirikiano na halmashauri kupitia idara ya maendeleo ya jamii na kuwa na katiba au muongozo utakaozimamia utekelezaji wa shughuli zote za jukwaa".

Aidha aliwataka wanajukwaa kuwa na ushirikiano wa karibu na uongozi wa wilaya na wasisite kuomba ushauri kwani viongozi wako kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wake wanafanikiwa kiuchumi na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya kila mtanzania kuwa na maisha bora hadi ifikapo 2025, hivyo bila ya ushirikiano na kuwasaidia wananchi kujua na kuzifahamu fursa mbali mbali za kiuchumi serikali haitaweza kufikia malengo.

"Nimeanza kufanya mawasiliano na shirika la viwanda vidogo (SIDO) kuona uwezekano wa upatikanaji wa mashine za kurahisisha kazi kama kubangua korosho, kupukuchua nafaka kama  mahindi, mbaazi, na ufuta kwa njia rahisi na kuepukana na utumiaji wa njia za asili ambapo mkulima anatumia nguvu na muda mwingi angali angeweza kufanya kazi nyingine za uzalishaji na kuongeza kipato"

Na kwa upande wa mbunge wa tunduru kusini Mh. Daimu Iddi Mpakate allisema kuwa umakini wa familia lazima uanze kwa mama kama akiwa legelege ataeweza kumsimamia mumewe hivyo kuwaomba kina mama kusimama imara katika jukwaa walilolianzsha na kuwa chanzo cha kuimarisha uchumi katika familia zao na kuongoza wanaume zao kwani serikali haitegemei mwanamke kuchukua mkopo na kwenda kumpa mumewe kuongeza mke mdogo bali kuanzisha biashara ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na hali ngumu ya maisha.

mkuu wa wilaya yaTunduru Mh Juma Zuberi Homera akifuatilia igizo wakati wa uzinduzi wa jukwaa la uwekezaji wanawake kiuchumi wilaya ya Tunduru uliofanyika katika ukumbi wa klasta ya mlingoti tarehe 15/08/2017

Alisema "sisi wabunge tuko tayari kuwaunga mkono na kwa kuanza tutahakikisha ofisi inapatikana pamoja na samani zake ili kuwezeshwa jukwaa hili kufanya kazi kwa wakati katika halmshauri yetu na niko tayari kwa kikundi chochote cha wanawake kitakachofika kuomba ushauri bila ya kujali wanatoka sehemu gani, naomba masuala ya kubaguana huyu wa huku na huyu wa kule tuyaache wanawake tuungane tuwe kitu kimoja"

Nao viongozi wa jukwaa la wanawake wakiongozwa na mwenyekiti mama Fatima Rajabu Mkina  waliushukuru uongozi wa wilaya kuzindua rasmi jukwaa hilo kwani ni muda mrefu sana wamesubiri chombo hicho kwa kitambo sasa hivyo kuanzishwa kwake kutaongeza hamasa kwa wanawake kushiriki katika shughuli za uchumi, biashara, upatikanaji wa mitaji, na kupitia sheria za nchi katika masuala ya Uchumi na jinsia ya kujitegemea kiuchumi.


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Mh. Sikudhani Chikambo akiongea na wanawake katika hafla ya uzinduzi wa jukwaa la uwekezaji wanawake kiuchumi wilaya.


Jukwaa la wanawake wakitoa igozo kwa mgeni rasmi lenye maudhui ya kuwaasa wanaume wanaovuja mali baada ya mavuno ya korosho na kusahau kuwekeza katika Elimu na kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kuongeza kipato cha familia na kuondokana na umaskini.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.