Shirika la maendeleo ya Nishati ya mafuta ya petroli Tanzania (TPDC) wamechangia milioni 25 ujenzi wa kituo cha afya Nakayaya wilayani Tunduru ikiwa kuunga mkono
juhudi za Mkuu wa wilaya hiyo Juma Zuberi Homera, katika kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya amabyo inazidiwa na wagonjwa kutokana na
ongezeko kubwa la wagonjwa na kupokea wagonjwa wa rufaha kutoka vijiji vya pembezoni.
Akizungumza na waandishi wa habari, wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa kukabidhi hundi hiyo kwaMkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera,
Mkurugenzi wa mawasiliano TPDC Bi Maria Mseremo kwa niaba ya mkurugenzi mkuu TPDC amesema kuwa shirika la maendele ya mafuta ya Petroli Tanzania (TPDC)
linafanya kazi katika mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na mkoa wa Ruvuma tumefika Wilaya ya Tunduru.
"tunakabidhi hudhi ya Milioni 25 ikiwa ni mchango wa kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Afya Nakayaya ili kupunguza kesi za wagonjwa kusafirishwa kwa
Wingi kwenda katika Hospitali za Masasi na Ndanda na kurahisha huduma karibu na wananchi walio wengi na kuungana na sera ya awamu ya tano ya
kuboresha huduma za afya " alisema Bi Maria Mseremo.
Mkurugenzi wa mawasialiano shirika la TPDC Bi Maria Mserema akizungumzaa na vyomba vya habari wakati wa kukabidhi hudhi ya milioni 25 iliyotolewa na shirika hilo katika kuchangia ujenzi wa kituo cha afya Nakayaya Wilayani Tunduru
Aliendelea kusema kuwa shirika linatoa huduma sehemu ambazo zina uhitaji lakini kwa sasa tupo katika mikoa ya kusinina tumefanya kazi kwa karibu na sana Mtwara na
Lindi katika kuboresha huduma za jamii.
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera ameshukuru na kupongeza moyo wa kujitoa na kushirikia katika shughuli za maendeleo
Shirika la TPDC kuona umuhimu wa kuchangia Wilaya zilizopo pembezoni mwa nchi kama Tunduru na kutoa rai kwa mashirika mengine kuiga Mfano wa TPDC
kwani wangeweza kwenda kutoa mchango katika mikoa kama Arusha, Mwanza na Dar es salaam.
"nimpongeze mkurugenzi wa Shirika la TPDC kwa mchango wa ujenzi wa Kituo cha Afya Nakayaya wa Milioni 25 kwani zimesaidia sana katika
kuendeleza na kuongeza kasi ya ujenzi huo hadi kufikia sasa ujenzi upo katika hatua za kuezeka"
Wakuu wa Idara na vitengo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera baada ya makabidhiano ya hundi ya kuchangia ujenzi wa kituo cha afya nakayaya na Mkurugenzi wa Mawasiliano TPDC mapema leo bi Maria Mserema aliyemuwakilisha Mkurugenzi mkuu TPDC.
Hata hivyo aliwakaribisha TPDC kuendelea kuchangia katika shughuli nyingine za kijamii kwani wilaya ya Tunduru ina mahitaji makubwa sana katika sekta mbalimbali ikiwemo michezo, elimu na nyinginezo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.