Akisoma taarifa ya Chama cha Ushirika Mnatinga katibu wa chama Ndg Mohamed Abdalah Arobaini alisema chama kina jumla ya wanachama wapatao 98 kutoka katika Kata nane za Namakambale, Ngapa, Tinginya, Mindu, Nakapanya, Mchuluka, Mtina na Chiwana.
Aliendelea kusema kuwa Amcos ya Mnatinga ina lengo la kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia 426 toka 98 wana sasa lakini chama kitakua kinafanya kazi ya kununua mazao Mchanganyiko na pia kutoka wigo wa kuanzisha kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta na Alzeti ilimradi kukuza uchumi wa wananchi.
Akizungumza na wanachama wa Amcos ya Mnatinga Mrajisi Msaidizi mkoa wa Ruvuma Bi Bumi Masuba alianza kwa kuwapongeza wanachama kufanikiwa kufikia malengo ya kuanzisha chombo ambacho kitawasaidia kupata nguvu ya kujiendeleza kwa mwananchama mmojammoja ili kutelekeza kauli mbiu ya ushirika tujenge uchumi wenye nguvu.
Katibu wa Amcos ya Mnatinga akisoma taarifa ya Chama hicho kwa wanachama na Mrajisi Msaidizi mkoa wa Ruvuma Bi Bumi Masuba katika mkutano maalum wa uchaguzi na kukabidhi cheti ulifanyika mapema wiki hii shule ya msingi Songambele wilayani Tunduru.
Bi Bumi Masuba alisema kuwa Mnatinga iki kufikia malengo waliyojiwekea ni wazima kusimamia Sheria ,kanuni na masharti ya ushirika nchini ikiwa ni pamoja na kuwa wanachama hai aliyelipa nusu ya hisa za uanachama.
Pia alikemea baadhi ya tabia za wanachama kutumia jazba au ushabiki katika kuchagua viongozi watakaosimamia ushirika kwani mkifanya hivyo wanamnatinga chama hiki tunachoenda kukizindua leo rasmi kitakufa mikononi mwenu.alisema "Mnatinga inajengwa na nyinyi wanachama wenyewe na mnatatinga itabomolewa na ninyi pia"
Bi Masuba aliwataka wanachama kutumia fursa ya serikali ya awamu ya tano katika kuimarisha ushirika kwani serikali ina nia njema katika kuimarisha ushirika nchini na imeweka mkazo katika usimamizi wa kukuza ushirika wenye nguvu nchini kwa ajili ya maendeleo ya Nchi na kukuza uchumi wa wananchi.
"Kuweni na mipaka katika utendaji kazi wa wanachama na masuala ya kisiasa ili kuepuka migogoro katika chama, vikao vyenu vinawahusu wanachama wenye hisa tuu na sio kila viongozi wa kisiasa, tunapojenga nyumba ni vizuri kuwa na misingi na mipaka"
Akitoa shukrani kwa wanachama baada ya uchaguzi mwenyekiti wa bodi ya chama cha ushirika cha Mnatinga Ndg Gerard Ford Richard alisema atatoa ushirikiano kwa bodi iliyokuwepo ili kuendeleza chama, atakua mtii kwa viongozi na wanachama na nitahakikisha hakuna makundi ili kuwaleta wanachama pamoja kama tulivyoanza mwanzo.
Mrajisi Mzaidizi Mkoa wa Ruvuma Bi Bumi Masuba akionesha cheti cha usajili wa chama cha Ushirika cha Mnatinga mbele ya wanachama na wajumbe wa bodi baada ya kufanya uchaguzi wa bodi mpya baada ya bodi ya mpito kumaliza muda wake.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.