• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

TASAF ILIVYOYABADILI MAISHA YA WALENGWA TUNDURU

Imewekwa : March 2nd, 2020

Mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Tunduru umebadili maisha ya wanufaika wilayani Tunduru ukilinganisha na walipokuwa wanaishi kabla ya mradi huu kuanza kutekelezwa mwaka 2014.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa mradi wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Ndg Muhidin Shaibu wakati alipotembelea kijiji cha Namakambale kuona maendeleo ya wanufaika wa mradi huo.

Alisema " tangu mradi umeanza mwaka 2014 kumekuwa na mabadiliko makubwa yamefikiwa kwenye kaya hizo ikiwemo kuongezeka kwa wanafunzi shuleni,kuhudhuria kliniki na kaya kuwa na uhakika wa kupata milo mitatu kwa siku tofauti na siku za nyuma hivyo kupungua kwa kiwango kikubwa tatizo la udumavu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano".

Aidha baadhi ya wanufaika wa mpango huo wameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za ruzuku ambazo zitawasaidia kuwajengea uwezo wa kiuchumi kwa kuanzisha biashara na kuwapatia kipato cha kila siku.

Akitoa ushuhuda wa namna mpango  huu ulivyomuwezesha kujikwamua kiuchumi Bi Mwajuma Kassima mnufaika kutoka kijiji cha Misufini Kata ya Namiungo amesema, licha ya TASAF  kumwezesha kupata kipato pia ameweza  kujenga nyumba ya vyumba vitatu anayoishi na familia yake." kabla sijaanza kupokea fedha za Tasaf nilikua  na maisha duni naishi  kwenye nyumba ndogo iliyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi jambo lililosababisha kudharaulika mbele ya jamii,lakini baada ya kuingia kwenye mpango nimekuwa  mtu mwenye amani katika maisha yangu na heshima kubwa".

Naye Bi Asha Mponda mnufaika kutoka kijiji cha Namakambale alisema TASAF imemwezesha kujenga nyumba ya kisasa,kusomesha watoto na kuweza kuanzisha mradi wa ufugaji ambapo mpaka sasa ana jumla ya Mbuzi nane, kumuongezea kipato na kuheshimika katika kijiji chao.

Kwa upande wa Mtendaji wa Kata ya Namakambale Bi.Hadija Lukanga alisema, kata hiyo ina kaya 391 waliopo katika mpango wa kunusuru kaya maskini kati ya hizo zipo kaya wapo ambao wameanzisha vikundi vya kuweka na kukopa pamoja na biashara ndogo ndogo.

Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa serikali na kusema kuwa  TASAF imesaidia sana kuboresha maisha ya wananchi wa kata hiyo kwani hata kiwango cha umaskini kimepungua sambamba na mahudhurio makubwa ya watoto shuleni ambao wote wanakwenda wakiwa na sare na mahitaji yote muhimu ikilinganisha kabla ya mpango kuanza utekelezaji.







Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.