Wilaya ya Tunduru imefanya ufunguzi wa minada ya uuzwaji zao la korosho ghafi kwa msimu wa 2023/2024, umefanyika Novemba 02, 2023 katika kata ya Nakapanya,Namitili AMCOS.
Minada ya korosho imefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Wakili, Julius S. Mtatiro. Katika hafla hiyo, wageni mbalimbali walihudhuria akiwemo, Mrajisi msaidizi wa Mkoa, meneja wa bodi ya korosho tawi la Tunduru, na katibu Tawala wa wilaya ya Tunduru.
Wakulima Wilayani Tunduru wameuza tani 5,300 za zao la korosho kwa bei ya wastani wa shilingi 1994 kwa kilo moja. Katika mnada huo, kampuni 39 zilionesha nia ya kutaka kununua Korosho zilizopo ghalani,ambapo kampuni 12 zilishinda.
Akizungumza katika ufunguzi wa mnada wa korosho Mhe. Wakili, Mtatiro aliwahimiza wakulima kupanua mashamba yao, na walime mazao yao kimkakati ili waweze kupata faida kubwa kupitia mazao. Awaonya vijana kuhusu uzururaji na kupenda kukaa vijiweni bila kufanya kazi.
“Vijana mna nguvu za kutosha, epukeni kukaa vijiweni na kufanya mambo yasiyo ya msingi, wekezeni nguvu zenu zote kwenye kilimo” Alisema, “Tunduru ni moja kati ya wilaya zinazoongoza kwa uzalishaji wa korosho nchini, mbolea inayouzwa nchini ina bei rafiki sana ukilinganisha na jinsi wanauza nchi nyingine,Tutumie fursa hii vizuri”
Mnada huo ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuboresha mfumo wa ununuzi kupitia stakabadhi ghalani. Mfumo huo mpya unalenga kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri za korosho.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.