Shule 10 za Sekondari zimeshiriki Tamasha la Tunduru Inter School Bash tarehe 23.09.2023 katika viwanja vya CCM vilivyopo Wilayani humo. Lengo kuu la Tamasha hili lilikuwa ni kuongeza ushirikiano na kuimarisha urafiki kati ya vijana hawa huku wakijifunza kutoka kwa wengine.
Tamasha hili lilijumuisha michezo mbalimbali kama vile Mpira wa Miguu, Wavu na Pete, Sanaa ikiwa ni pamoja na Kuimba, Kucheza, Mitindo na Ngoma. Katika taaluma, Wanafunzi kutoka Shule hizo walishiriki kujibu mashindano ya maswali ya masomo mbalimbali.
Aidha, Tamasha hili lilijumuisha shughuli ya uchangiaji damu lililoratibiwa na Hospitali ya Wilaya ya Tunduru kwa kushirikiana na Shule za Sekondari zilizoshiriki katika tamasha hilo. Shughuli hiyo ilifanikiwa kukusanya Chupa 14 za damu ambazo zitatumika kuokoa maisha ya mama na mtoto. Pia, Mtaalamu wa Lishe aliratibu zoezi la kutoa Elimu na Ushauri kwa vijana wa rika Balehe na walipimwa hali zao za Lishe.
Tamasha hilo litaendelea kukuza umoja na ushikiano kati ya vijana kutoka Shule mbalimbali za Sekondari Wilayani Tunduru. Pia, litahamasisha vijana kuhusu umuhimu wa kujitolea na kusaidia jamii.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano serikalini Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.