Tunduru 03 April 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani Tunduru kuanzia tarehe 04-05 April 2019.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe.Juma Zuberi Homera inasema, barabara ya lami ya Namtumbo āKilimesera,Matemanga-Tunduru itakaguliwa na kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais.
Katika ziara hii Mhe.Rais Magufuli ataongea na wananchi katika viwanja vya soko la Mchele lililopo Nakayaya Tunduru Mjini.
Wito unatolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi kuanzia Kijiji cha Sauti Moja, Nakapanya, Muhuwesi siku ya Tarehe 04/04/2019 hadi Eneo la Mkutano wa hadhara Nakayaya siku ya tarehe 05 Aprili, 2019 kuanzia saa mbili kamili Asubuhi.
Imetolewa na
Theresia E.Mallya
Afisa Habari
Halmashauri ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
HakimilikiĀ©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.