Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Wakili Julius S. Mtatiro anawatangazia wafanyabiashara wa sukari wa jumla na rejareja, kuacha mara moja kuuza sukari kwa bei isiyokuwa elekezi.
Pichani: Mhe. Wakili Mtatiro akizungumza na Mfanyabiashara wa duka la reja reja, alipofanya ukaguzi wa kushtukiza kukagua Bei ya Sukari maeneo mbalimbali.
Kwa mujibu wa amri ya serikali iliyotolewa kupitia tangazo la serikali namba 40b la tarehe 23.01.2024, bei ya sukari kwa mkoa wa ruvuma na wilaya zake zote ni kama ifuatavyo; a. Bei ya rejareja kwa maduka ya rejareja ni shs. 2,900 - 3,200 kwa kilo moja (1). B. Bei ya jumla kwa sukari iliyo kwenye mfuko wa kilo 20 ni shs. 53,000 hadi shs 58,000. C. Bei ya jumla kwa sukari iliyo kwenye mfuko wa kilo 25 ni shs. 66,250 hadi shs. 72,500.
Mkuu wa wilaya amebaini wako wafanyabiashara wanauza sukari kwa bei zinazokiuka amri ya serikali ambayo inatokana na msingi wa bei walizonunulia viwandani, gharama za usafirishaji na faida.
Mkuu wa wilaya anaagiza wafanyabiashara wote wa jumla na rejareja kuuza sukari kwa bei ya haki na bei elekezi mara moja, pia, anaagiza maduka yote ya jumla na rejareja kuweka vibao vya bei elekezi za sukari mara moja, duka litakalokutwa halina kibao cha bei elekezi sehemu ya wazi litachukuliwa hatua kali.
Mwananchi atakayeuziwa sukari tofauti na bei ya shs 2,900 - 3,200 kwa kilo atoe taarifa mara moja kwenye namba ya mkuu wa wilaya 0739420421.
Mfanyabiashara atakayekiuka tangazo hili, atachukuliwa hatua kali.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.