Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za sikukuu ya Krismasi kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru. Salamu hizi zinalenga kuwatakia wananchi furaha na amani katika kipindi hiki cha sikukuu.
Katika salamu hizo, Rais Samia ametoa zawadi mbalimbali kwa wananchi, hasa wale waliopo kwenye makundi maalum. Zawadi hizi zimewasilishwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Ndg. Milongo Sanga,ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru.
Pichani (kushoto)ni Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Ndg. Milongo Sanga,ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru akikabidhi moja ya zawadi hizo.
Ndg. Sanga alisema Zawadi hizi zimeandaliwa ili kuwasaidia wananchi hawa kusherehekea sikukuu ya Krismasi kwa furaha na kwa njia inayofaa. Pia, zinatarajiwa kuwawezesha wananchi wa Tunduru kusherehekea sikukuu kwa njia ambayo itawapa faraja na kuimarisha umoja miongoni mwao.
"Ni hatua ya kuonyesha upendo na mshikamano wa kitaifa, hasa kwa wale wanaohitaji msaada zaidi katika jamii" Alisema Ndg. Sanga "Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuimarisha ustawi wa jamii na kusaidia makundi maalum, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto, na wazee".
Salamu za sikukuu na zawadi hizo ni ishara ya uongozi wa Rais Samia katika kuimarisha mshikamano na kusaidia wananchi, hasa katika nyakati za sherehe na furaha.
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru wanatarajiwa kufurahia sikukuu hii kwa pamoja tarehe 25.12.2024, wakikumbushwa umuhimu wa kusaidiana na kuungana kama jamii.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.