Halmashauri ya wilaya ya Tunduru katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 ilitenga Tsh milioni 46,700,000 kununua kifaa cha kupimia ardhi cha aina ya RTK GPS kitakachutumika kupima viwanja wilayani Tunduru kwa mpango wa upimaji shirikishi.
Akiongea baada ya kupokea vifaa hivyo mapema leo mpima ardhi wilaya Ndg Jeremieh Fredrick Nhambu amesema kununuliwa kwa kifaa hicho kutarahisha kazi ya upimaji wa viwanja kwa wananchi kutokana na kifaa walichokuwa wanatumia awali kilikua kimoja tuu na kichakavu hivyo kununuliwa kwake kutaboresha zoezi la upimaji.
Mwakilishi wa Kampuni yaSESCLEA Ndg Haji Mchatta akitoa mafunzo kwa watumishi wa Idara ya Ardhi Kitengo cha Mipango Miji na Upimaji wakati wa makabidhiano ya kifaa kipya cha kupima viwanja yalifanyika katika ofisi za Idara ya Ardhi na Maliasili Halmashauri ya Tunduru mapema leo hii.
Watumishi wa ardhi wakipata mafunzo na maelekezo ya namna ya kutumia kifaa kipya cha RTK GPS kutoka kwa mhandisi wa Kampumi ya SESCLEA baada ya makabidhiano ya kifaa hicho Tunduru kilichonunuliwa kupitia makusanyo ya ndani.
Wapima Ardhi wilaya wakifanyia majaribio kifaa kipya cha kupimia viwanja cha RTK GPS kuona namna kinavyofanya kazi. aliyeshika pointer ni Mpima Ardhi Wilaya Jeremieh Nhambu akiwa pamoja na watumishi wa Idara ya Ardhi na Maliasili pamoja na Afisa Ugavi Ndg Paul Riziki aliyekuwa akifanya uhakiki wa vifaa hivyo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.