Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme katika kikao cha tathimini ya uuzaji wa zao la korosho kwa msimu wa korosho mwaka 2017/2018, ambapo changamoto za baadhi ya wakulima hawajalipwa fedha kutokana na baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi kufanya udanganyifu na kuwalipa wakulima mara mbili.
Akizungimza katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa klasta ya mlingoti mapema wiki hii Bi Mndeme amesema kuwa kuna jumla ya wakulima wapatao 178 ambao wanadai vyama vya msingi jumla ya milioni 143,182,670.63 fedha ambazo baadhi ya waandishi wa vyama vya msingi walijilipa wenyewe na wengine kuwalipa wakulima mara mbili hivyo kuleta usumbufu kwa serikali na wananchi.
Bi mndeme alisema “ninatoa siku saba (7) tuu kwa wakulima walioingiziwa fedha za korosho mara mbili kwa makosa ndani ya katika akaunti zao kuhakikisha kuwa wanazirejesha ili walipwe wakulima ambao hawajalipwa fedha zao”.
viongozi wa vyama vya msingi wakifuatilia mkutano wa tathimini ya uuzaji wa zao la korosho mkoa wa Ruvuma katika msimu wa korosho mwaka 2017/2018.
Vilevile kwa viongozi wa vyama vya msingi aliwataka ndani ya siku saba wawe wamerejesha fedha zote za wakulima ambazo hawajalipa mpaka sasa, na kwa wale ambao hawatatekeleza kwa wakati serikali haitosita kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwapeleka mahakamani na kuwafungulia kesi. alisema Bi Mndeme.
Huku mwandishi wa Maji Maji Amcos akikabidhiwa kwa mkuu wa Jeshi la polisi Mkoa kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano baada ya kubainika kujiingizia fedha za wakulima milioni 72 katika akaunti yake binafsi kinyume cha sheria.
Hata hivyo alimalizia kwa kuvitaka vyama vyote vya msingi vya ushirika wilayani Tunduru kuajiri waandishi ambao ni wazalendo na wanaojali maslahi ya wakulima ili kuepukana na watu wachache wenye tamaa ya kuwaibia wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.