• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Benki ya Posta wawezesha vifaa saidizi kwa watoto wenye Ualibino Tunduru

Imewekwa : June 9th, 2019

Benki ya posta Tanzania Tawi la Tunduru imekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 2,949,000.00 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi waliopo katika shule za msingi na sekondari wilayani Tunduru.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru  Ndg Gasper Balyomi Meneja wa Benki ya Posta tawi la Tunduru Bi. Emajackline Mtemba alisema vifaa hivyo ni mafuta kinga, kofia za kujikinga na mionzi ya  jua (pama), Miwani, Sabuni za kuoga, na Viookuza (Magnifier).

Bi Mtemba aliwaasa watoto hao kutumia vifaa hivyo kusoma vizuri na kuwa chachu ya kuongeza bidii katika masomo yao,kuweni na  nidhamu kwa  kutii wazazi na walimu “lakini vifaa hivi viwe chachu kwenu ya kusoma na kufanya vizuri Zaidi kwenye masomo yenu kwani nyie ndio viongozi wa baadaye na ni matarajio ya benki ya posta ya Tanzania kuwa watoto hawa wenye ulemavu wa ngozi wana nafasi kwenye jamii kama walivyo watoto wengine na ndio viongozi wa baadaye”

Nitoe wito kwa wazazi wote kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu wa ngozi kwani wao wana haki ya kupata elimu kwani ni haki ya msingi kwa kila mtoto na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inawatambua na kuwajali, pia niwakumbushe wazazi kuwawekea watoto Amana kwa ajili ya kusomea ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa Ada.

katika picha ni meneja wa benki ya posta tawi la Tunduru na Mkurugenzi Mtendaji Ndg Gasper Balyomi aliyeshikilia kiookuza (magnifier) wakikabidhi vifaa hivyo kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru

Akitoa taarifa fupi ya Halmashauri ya Tunduru  mgeni rasmi ambaye pia Mkurugenzi Mtendaji  Ndg. Gasper Zahaoro Balyomi alianza kwa kuishukuru benki ya posta Tanzania  tawi la Tunduru kutoa vifaa saidizi kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru ambapo alipokea kofia 72, mafuta kinga chupa 72, sabuni 72, miwani na viookuza kwa ajili ya kugawa kwa wanafunzi hao.

Gasper Balyomi aliendelea kusema Halmashauri ya Tunduru ina shule 149 za serikali kati ya hizo  shule mbili tuu ndio zina  vitengo vya elimu maalum, ambazo ni  Tunduru Mchanganyiko na Namiungo shule ya Msingi.

“Tunduru ina shule za msingi 149 za serikali na shule mbili za Namiungo na Tunduru Mchanganyiko ndio wanapokea watoto wenye mahitaji maalum, lakini ina idadi ya wanafunzi wenye ulemavu  432 ikiwa wasichana ni 167 na wavulana 265, na upande wa shule za sekondari ina wanafunzi 27, wasichana 12 na wavulana 15, lakini watoto wenye ulemavu wa ngozi ni 36 ikiwa wasichana ni 19 na wavulana 17”alisema Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru.

Aidha alisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo watoto hawa wenye ulemavu wa ngozi ni pamoja na kukosekana kwa mafuta kinga, miwani, kofia za kujikinga na mionzi ya jua (Pama), lakini pia kukosekana kwa huduma za matitabu ya ngozi katika hospitali za wilaya na badala yake zinapatikana katika hospitali zenye vitengo maalumu kama hospitali KCMC iliyopo Moshi, Bugando mwanza na Muhimbili ambapo wazazi wanashindwa kumudu gharama za kuwasafirisha watoto hawa.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri  ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi akimvisha kofia ya kujikinga na mionzi ya jua (pama) mmoja wa watoto wakati alipokua akipokea vifaa kutoka kwa meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduru Bi.Emajackline Mtemba  vyenye thamani Tsh 2949,000.00 katika halfa iliyofanyika ukumbu wa klasta.

Aliendelea kutanabaisha kwa  kusema  Halmashauri ina walemavu wa aina mbalimbali hivyo ni vyema jamii na wadau wa maendeleo kujitokeza katika kuwawesha ili waweze kusoma na kufikia malengo yao kwani miongoni mwa hawa watoto wapo wenye vipaji ambavyo vinahitaji kuendelezwa.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa Halmashauri ina mpango mkakati wa  kuanzisha  shule ya watoto wenye mahitaji maalum kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari ambao wakifaulu wanashindwa kuendelea na masomo.

Sambamba na kuanzishwa  kwa shule hiyo  lakini kwa sasa tuna mikakati ya kuiombea shule ya sekondari Nandembo iliyopo wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma kuanzisha  kitengo cha Elimu maalum ili kupunguza changamoto ya wanafunzi wanaofaulu kuendelea na masomo ya juu kutumia nafasi zao kwani wengi wanashindwa kwenda shule wanazopangiwa nje ya wilaya kutokana na wazazi kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Halmshauri ya Tunduru Kaimu afisa elimu Bi Loya Mwajabu kwa Benki ya Posta Tawi la Tunduru alisema  serikali kupitia  sera ya elimu ya mwaka 2004 haijabagua watoto kwani watoto wote ni sawa na wanatakiwa kupata elimu kwani ni haki ya msingi.

watoto wakimsikiliza mgeni rasmi ambaye ni mkurugenzi mtendaji  halmashauri ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi ambaye hayupo katika picha wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa saidizi kutoka benki ya posta tanzania tawi la Tunduru,

Alisema Kupata elimu kwa watoto kutamsaidia mtoto kujitambua na kupata urithi ulio sahihi, mama ni mlezi mkubwa na nikuhakikishie kuwa hawa watoto watatumia vifaa hivi vile iliyoelekezwa, wito wetu kwa jamii ni kuwa  hawa wamezaliwa hivi walivyo na wana haki ya kupata elimu kwani ndio ukombozi wao.

Aidha niwaombe wazazi,  jamii na wadau wa elimu na maendeleo ndani nan je ya wilaya ya Tunduru kuguswa na watoto hawa, kuunga mkono juhudi za serikali katika  kuwasaidia vifaa saidizi watoto kwani watoto 432 wenye ulemavu ni wengi sana na sio hawa wenye ulemavu wa ngozi tuu,pia wapo wenye mtindio wa ubongo, bubu viziwi, viwete na wote hawa wanahitaji kusaidiwa kufikia ndoto zao.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.