Akiwa katika ziara ya ukaguzi mwenendo wa ujenzi wa majengo katika vituo vya afya Matemanga na Mkasale Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Naibu waziri ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh.Josephat Kandege alisema serikali imetoa milioni 500 katika kituo cha Afya matemanga na 400 katika kituo cha afya Mkasale ili kuhakikisha kwa huduma za afya zinaboreshwa.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh.Josephat Kandege katika ziara ya ukaguzi wa ukarabati wa miundombinu ya majengo katika kituo cha afya Matemanga mapema wiki.
Akizungumza na viongozi wa mkoa,wilaya pamoja na wananchi wanaozunguka kituo cha afya Matemanga alisema eneo la kituo cha afya Matemanga ni dogo na majengo yake yanakaribiana na makazi ya wananchi hivyo ni vyema serikali kuchukua hatua za makusudi za kulipa fidia stahiki kwa wananchi ili kupisha eneo hilo.
Naibu waziri Kandege amesema majengo ya kituo cha afya kukaribiana sana na wananchi makazi ya wananchi ni hatari wakati wa magonjwa ya mlipuko na hata mionzi inayotoka katika chumba cha mionzi ni hatari kwa afya za wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg Chiza MArando akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akiwa katika ziara ya ukaguzi mwenendo wa ujenzi wa upanuzi wa majengo ya Kituo cha afya Matemanga.
Akielezea kuhusu eneo la kituo cha Afya Mh. Kandege alisema kuwa eneo la kituo cha afya linatakiwa kuwa na ukubwa wa ekari nane na kuendelea hivyo ni jukumu la mkoa kushirikiana na halmashauri ya Tunduru kuhakikisha kuwa wanatwaa maeneo kuzunguka kituo hicho.
“viongozi wa mkoa simamieni upatikanaji wa ekari nne zaidi ili kuwe na eneo la ekari nane kulingana na mahitaji ya eneo la ujenzi wa vituo vya afya, wananchi nawaomba kuachia maeneo na serikali ya kijiji fanyeni mpango wa kuwapatia maeneo mengine”
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege (wa pili kutoka kushoto) akikagua mtambo wa uliotumiwa na halmashauri katika kufyatua tofali za ujenzi wa majengo katika vituo vya afya Matemanga na Mkasale akiwa katika ziara
Hata hivyo aliwasisitiza wananchi wa Tunduru kujitokeza kwa wingi kujiunga na mfuko wa bima ya afya jamii iliyoboreshwa (ICHF) ili kuweza kupata matibabu yenye uhakika kwa kaya watu sita kwa kipindi cha mwaka mzima kwa shilingi elfu 30 tuu. “bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa inakuwezesha kupata matibabu katika hospitali ya wilaya, kituo cha afya na hospitali ya mkoa kwa elfu 30 tuu.”
Naibu waziri kandege amehitimisha ziara mkoani Ruvuma katika wilaya ya Tunduru ya kufanya ukaguzi wa ukarabati wa vituo vya afya na kutoa maagizo ya ujenzi wa majengo kulingana na maelekezo yanayotolewa, pia kuhakikisha kuwa kila kituo cha afya kinajenga jengo la mionzi (Ultrasound) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya mama wajawazito.
Imetolewa na
Theresia Mallya
Afisa Habari Halmashauri Tunduru
Simu 0764287387
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.