Hayo yamesemwa na naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk Hamisi Kigwangala akiwa katika ziara ukagazi wa utekelezajiwa agizo la uboreshaji wa vituo vya afya katika kila kata nchini lilitolewa desemba 2016.
Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Tunduru wakati ziara Dk Kigwangala amesema serikali inaendelea na uboreshaji wa huduma za afya na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zenye ubora na kwa wakati na lengo la serikali ya awamu ya tano ni kupunguza kwa asilimia kubwa changamoto zinazoikabili wilaya ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, kukamilisha maboma yote ya vituo vya afya, zahanati na hospitali ambazo hazijakamilika, na kuhakikisha kuwa vifaa tiba na dawa zinapatikana za kutosha.
Aliendelea kusema kuwa ili mwananchi aweze kushiriki katika shughuliza uzalishaji ni lazima awe na afya njema na ili awe na afya njema ni lazima wananchi kwa kushirikiana na serikali kuboresha vituo vya kutoa huduma za afya na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kuwa dawa zinakuwepo za kutosha katika hospitali na vituo vya afya na katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imetenga bajeti ya kutosha kuhakikisha kuwa vifaa tiba vinakuwepo katika vituo vya afya na hospitali zote nchini.
Samabamba na hayo serikali inahakikisha kuwa huduma za mama na mtoto zinatolewa bure kwenye hospitali za umma zote nchi ili kupunguza vifo vya wamama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Dk Kigwangala aliuagiza uongozi wa kijiji cha mkasale na mkotamo kutengeza barabara ya kuelekea katika kituo cha afya mkasale kutoka na barabara hivyo kuwa chafu sana hali inayoweza kuleta madhara kwa watumiaji hasa kwa wadudu kama nyoka.
"nakuagiza mwenyekiti wa kijiji mara baada ya kumaliza kikao hapa upange ratiba na wananchi wako namna bora ya kuweza kutengeza barabara inayokwenda katika kituo cha afya mkasale na pia mupange ratiba ya kufanya ausafi katika kituo kwani kazi ya usafi ni ya wananchi"alisema dk kigwangala.
viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru wakiwa katika mapokezi ya Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia,Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk Hamisi Kigwangala ambaye hayupo katika picha.
Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zilizo bora uongozi wa wilaya unatakiwa kufanya yafuatayo katika vituo vyote vya afya vilivyopo wilayani Tunduru, kujenga vyumba vya upasuaji katika vituo vyote vya afya, kukarabati maabara zote,na kuhakikisha kunakuwepo na mfumo wa maji safi wenye uhakika katika vituo vyote vya afya, kufanya matengenezo kwa vifaa vilivopata hitilafu ili kuboresha huduma.
Hata hivyo nawasihi wananchi tumuunge mkono raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania dk John Pombe Magufuli kwa vita aliyoianzisha ya kulinda rasilimali za nchi yetu, kwani taifa limekuwa likiibiwa kwa muda mrefu sana ila umefika muda kuhakikisha kuwa rasimali za nchi zinatunzwa na kulindwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.