Mwenyekiti msaidizi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Mh. Saidi Bwanali alihutubia katika uzinduzi huo wa siku kumi na sita (16) za kupinga ukatili kwa wanawake na watoto, katika wilaya ya Tunduru kata ya jakika katika kijiji cha kajima , katika hotuba yake mwenyekiti wa Halmashauri aliongelea masuala mbalimbali yatakayo wajenga katika kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto .
Mwenyekiti aliwaomba wazazi kuwalea watoto wao katika malezi ya kidini ili watoto hao wawe katika maaadili mema na mazuri ambayo yatawaoelekea kupata kizazi chema kwa baadae, na kuwasihi wazazi kuwapa mahitaji bora ambayo mtoto anatakiwa kupewa kama vile haki ya elimu .
Pia aliwaomba wakina baba kuwatunza wake zao kwa kuwapa mahitaji yote ambayo wanahitajika kutoa kwao , na kuwataka wakina baba kukomesha kabiza vitendo vya kuwafanyia ukatili wanawake kw kuwapiga ama ukatili mwingine wowote ule katika familia zao.
Pia mwenyekiti aliwataka wanawake/wanakina mama kuwaheshimu waume zao na kuwapa yale yote yanayaostahiki katika ndoa na familia zao , akawataka pia wanawake kutunza watoto wao hata kama ni watoto wa kufikia kwa baba ili waweze kuwasaidia baadae katika maisha yao.
Aidha mwenyekiti alisisitiza usawa katika familia hasa katika kutoa mawazo katika familia ili kujenga familia iliyo bora na imara katika maamuzi ya kifamilia
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.