Mh. Hairu Hemedi Mussa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru amefanya kikao na Viongozi wa Kata na Kijiji cha Tinginya ,Lengo la ziara yake ni kukagua eneo lililo tengwa kwajili ya Ujenzi wa Mkondo 1 wa Shule ya msingi Tinginya ambayo imepata Tzs 331,600,000/= kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa Kuboresha upatikanaji wa Fursa sawa katika ujifunzaji bora wa elimu ya awali na msingi Tanzania Bara (BOOST) ambapo aliwaambia wajumbe kuwa fedha hiyo sio nyingi kama wengi tunavyofikiria kwahiyo 20% ya Nguvu za Wananchi zinaitajika ili kuwezesha mradi ukamilike kwa Wakati pia aliwakumbusha Wajumbe wa Kamati Mbalimbali kufanya majukumu yao kwa weledi ikiwemo kutunza Vifaa na kuwasimamia vizuri Mafundi,Mh Hairu Mussa alishiriki kufanya usafi wa kukata miti na kuchimba visiki eneo ambalo mradi utajengwa.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.