Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, amewasili katika Wilaya ya Tunduru kwa ziara yake Mkoani Ruvuma, ambapo ametoa wito kwa wananchi kuendeleza misingi ya amani, upendo na unyenyekevu katika maisha yao ya kila siku.
Akiwahutubia waumini na wananchi katika mkutano uliofanyika katika viwanja baraza la Idd Tunduru, Mufti Zubeir ameeleza kuwa mmomonyoko wa maadili unaonekana katika jamii ni changamoto inayohitaji juhudi za pamoja kutoka kwa viongozi wa dini, serikali, na wazazi ili kurejesha maadili mema kwa vijana na familia kwa ujumla.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani hasa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, akiwataka wananchi kushiriki kwa amani, utulivu na kuzingatia sheria bila kujihusisha na vitendo vya vurugu au chuki.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.