Asasi ya kiraia COUNSENUTH ambao ni wasimamizi wa utekelezaji wa mradi wa Kijana Jiongeze kwa kushirikiana na Halmashauri kupitia ufadhili wa MasterCard Foundation imekabidhi vifaa vya michezo kwa shule 23 za Sekondari zilizopo Wilayani Tunduru.
Akikabidhi vifaa hivyo katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bi. Edina Obed Mgunda, ambaye ni Mratibu wa Mradi wa Kijana Jiongeze awamu ya pili, amesema vifaa hivyo vya michezo ni kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi huo katika kuchangia jitihada za shule za Serikali ili kuboresha michezo mashuleni, na hivyo, kuboresha hali ya mahudhurio na utayari wa kusoma na kupenda shule.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru (Kulia) Ndg. Chiza Marando akikabidhiwa Vifaa vya Michezo na Mratibu wa Mradi wa Kijana Jiongeze Bi. Edina Mgunda
“Mradi umepanga kufanya mashindano ya michezo na taaluma katika shule za Sekondari 23 ambazo mradi huu unatelekezwa”. Alisema “Vifaa hivi vya Michezo vitaongeza chachu ya wanafunzi kupenda shule, lakini pia kupenda Elimu, sisi kama wadau wa Elimu tunaamini kuwa michezo inaweza kuongeza kujifunza na kumvutia mwanafunzi kubaki shuleni” Alisema.
Vifaa vya michezo vilivyokabidhiwa ni Seti 14 za Jezi na mipira 46, ambapo, Seti saba za jezi ni kwa ajili ya timu saba za mpira wa miguu na saba kwa mpira wa pete, mipira 23 ni kwa ajili ya mpira wa miguu na 23 mpira wa pete.
(kushoto) Afisa Elimu Sekondari Mwal. Patrick Haule akipokea Vifaa vya Michezo
COUNSENUTH kwa kushirikiana na Idara ya Elimu Sekondari ya Wilaya ya Tunduru inatekeleza mradi wa KIJANA JIONGEZE wenye lengo kuu la kukabiliana na changamoto za ufaulu wa na kuhusisha njia za kuwawezesha wasichana kuwa na stadi za maisha zitakazowasaidia kutambua uwezo wazo, kujiamini na kuwaandaa kwa ajili ya ajira na kujiajiri. Mradi huu unatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, kwa ufadhili wa MasterCard Foundation.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.