Msimu wa Korosho waanza kwa kishindo Wilayani Tunduru.
Msimu wa ununuzi wa zao korosho wilayani Tunduru kwa mwaka 2017/2018 umeanza kwa kasi nzuri ya mnada wa kwanza kufunguliwa mapema leo katika Kijiji cha Namakambale tarafa ya Nakapanya mkoa wa Ruvuma na mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh. Juma Zuberi Homera.
Ununuzi na uuzaji wa zao la korosho umeanza kwa kasi nzuri ukilinganisha na miaka mingine kwa bei ya juu kwa kilo tsh 3,950 kwa mnada wa leo wa tarehe 02/11/2017, ikiwa ni bei kubwa kwa msimu huu toka uanza.
Jumla ya wafanyabiashara waliowasilisha zabuni (tender) ni 17 lakini walishiriki katika mnada ni 14 za wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi na kampuni ya Korosho Africa Ltd ndio iliyoshinda tenda leo kwa kununua kilo 544,000 kwa Ths 3,950 sawa na Tan 544 za korosho ghafi zilizokuwa ghalani ni kilo 544,144.
Akifungua mnada wa leo mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Tunduru TAMCU ltd Ndg Hashim Twalib Mbalabala alisema zoezi hili linafanyika kwa uwazi ili kuondoa migogoro miongoni mwa wakulima, serikali na vyama vya msingi.
Aidha akisoma taarifa kabla ya mnada afisa ushirika wilaya Ndg Peter Malekela alisema makato ya kisheria yatakatwa ikiwa ni ushuru wa Amcos sh 90, Mfuko wa wakfu -CDTIF sh 10, ushuru wa Halmashauri 43.5, mchango wa Elimu sh 50 na gharama za usafiri sh 50.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Zuberi Homera akiongea na wananchi wa wilaya ya Tunduru katika ufunguzi wa mnada wa kwanza wa korosho uliofanyika katika kijiji cha Namakambale wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma
Mkuu wa wilaya ya Tunduru ambaye alikuwa mgeni wa heshima katika ufunguzi wa mnada wa kwanza alisema bei ni kubwa toka msimu umeanza na korosho leo imeuzwa kwa bei ya shilingi 3950 ikiwa ni ongezeko la shilingi 200 ya bei ya msimu ulipita ambapo mnada wa kwanza ulinzakwa shilingi 3750.
Aidha Mh. Homera alimshukuru rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kuwezesha na kuramisha mfumo wa stakabadhi ghalani na kutoa kipaumbele kwa zao la korosho kuwa la biashara.
“Naishukuru serikali kutoa wigo mpana kwa zao la korosho na kuwa la kipaumbele na pia kuruhusu wanunuzi kutoka nje ya nchi kuja kununua korosho yetu”
Na kwa upande wa wananchi wa Kijiji cha Namakambale wameomba kuongezwa kwa magari ya kusafirisha korosho kutoka katika vyama vya msingi na kupeleka na ghala kuu la Tamcu lililopo Tunduru mjini.
Afisa Ushirika Wilaya Ndugu Peter Malekela wakisoma Tenda za wanunuzi wa Korosho mara baada ya kufunguliwa kwa sanduku la Tenda leo katika mnada wa kwanza uliofanyika katika kijiji cha Namakambale wilayani Tunduru
Hata mnada huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Tunduru wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh. Juma Zuberi Homera , kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) Ndg Chiza Marando ambaye ni Afisa Kilimo Wilaya, Mwenyekiti wa chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU) Bw Hashim Twalib Mbalabala na wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.