Mkuu wa wilaya ya Tunduru ndg Julius mtatiro alihudhuria mkutano uliohusu kutatua mgogoro uliokuwa baina ya mwajili wa wa kampuni ya korosho Africa na waajiliwa wake.
Mkuu wa wilaya aliundas kamati iliyofatilia mgogoro huo na kugundua kuwa kampuni ya korosho Africa ilikua na upungufu katika sehemu mbalimbali za kampuni hiyo hasa katika mikataba na wafanya kazi kuanzia mwaka 2009 hadi 202 ambayo inahusu
Malipo Ufanyaji kazi na malipo ya wafanya kazi ya siku kwa mda ambao kila mfanya kazi alifanya na muda ambao alifanya kazi
Kamati ilibaini pia mwajili wa kiwanda cha korosho afrika ana tatizo katika eneo la menejimenti na utumishi ,kama vile utunzaji wa nyaraka pia na utekelekezaji wa majukumu ya kiutumishi katika kampuni hiyo
Kamati ilibaini pia wafanyakazi wa kiwanda cha korosho afrika walisitishiwa ajira zao bila kupewa notisi tangu September 2020 bila kufuata mujibu wa mkataba ulivyokubaliana wa kupewa notisi ndani ya siku28.ambalo ni kosa kisheria
Kwahiyo ,mkuu wa wilaya ameipatia Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya korosho afrika siku 14 za kuweza kujadiliana na kutoa maamuzi juu ya madai ya waajili wao ambayo walikuwa wanaidai kampuni hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.