Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe.Wakili.Julius S. Mtatiro ahimiza watoto kuandikishwa shuleni, abainisha kuwa elimu ni msingi wa mustakabali wa watoto na maendeleo ya jamii kwa ujumla.watoto wanaopata elimu wanakuwa na uwezo mkubwa wa kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwa raia mwema katika jamii. Pia, asisitiza kuwa elimu ni njia ya kupambana na ujinga na umaskini ili kuwezesha maendeleo endelevu katika Wilaya yetu.
“Serikali inatoa fedha nyingi ili kuboresha miundombinu ya shule, kutoa vifaa vya kufundishia pamoja na kujifunzia” alisema Mhe.Wakili Mtatiro “Ni jukumu letu sote kuhakikisha watoto wanaandikishwa ili wapate elimu bora”
Aidha, Mhe.Wakili Mtatiro awahimiza wazazi kuchukua jukumu la kuwaandikisha watoto wao shuleni. Akumbusha wazazi kuwa elimu ni haki ya kila mtoto na ni jukumu lao kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu bora.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.