Mkuu wa wilaya ya Tunduru ndg Julius mtatiro ,alizungumza katika mkutano huo uliokusanya wadau wa zao la korosho , Mkuu wa wilaya ya Tunduru alizungumzia hasa kufanya marekebisho na kutatua changamoto zote ambazo zilisumbua msimu uliopita wa mwaka 2020/2021.
Pia mkuu wa wilaya alisisittiza kuhusiana na mfumo wa stakabadhi gharani ambao ambao amesema ni mfumo uliokuwa na tija kwa wakulima kwa kiasi kikubwa na kupiga vita biashara holela za mazao ya biashara katika wilaya ya Tunduru .
Katika msimu wa mwaka uliopita wa 2020/2021, chama cha ushirika cha Tunduru (TAMCU), ilifanikiwa kukusanya korosho kwa kiasi cha kilo 15,410. Ambacho ni makusanyo ya wilaya ya Tunduru na maeneo mengine ambayo yanauzia zao hili katika wilaya ya Tunduru ambayo ni Mbeya na njombe, katika msimu uliopita shirika lilitumia mfumo wa stakabadhi na katika minada walitumia mifumo miwili ambayo ni mfumo wa kielectronic na mfumo wa masanduku.
Katika mkutano huo mwenyekiti wa chama cha ushirika wilaya ya Tunduru ndg alitoa taarifa ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2021/2022 ambayo yamefanywa na chama hicho, ambayo ni, utengenezaji wa mizani ,magunia ya kuhifadhia mazao ambayo yanaweza kuhifadhi tani 16.
Kuna baadhi ya changamoto ambazo zilitakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka ambazo zilikuwa zinawakumba wakulima kama vile kushuka kwa bei ya mazao,ucheleweshaji wa malipo kwa wakulimu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.