Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Ndg. Chiza Marando, ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha watoto wao wanapelekwa shule ili kujenga msingi imara wa maendeleo kwa familia na taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo, Oktoba 8, 2025, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Machemba, Tarafa ya Nampungu, ambapo alisisitiza kuwa elimu ndiyo silaha pekee ya kupambana na umaskini na kuleta ustawi wa jamii.
Ndg. Marando amewataka wazazi na walezi kuacha visingizio na kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya msingi ya elimu, huku akiahidi kuwa Serikali kupitia Halmashauri itaendelea kuboresha miundombinu ya shule na mazingira ya kujifunzia.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.