Halmashauri ya wilaya ya Tunduuru kupitia Kitengo cha Tasaf inafanya malipo ya Tasaf kwa mwezi wa Saba na WaNane ambapo jumla ya Milioni 955 zinagawiwa kwa Walengwa wa Tasaf kati ya Walengwa kaya 21,6054 ambapo 16,610 Watalipwa keshi na walengwa 5,044 watalipwa kwa njia ya Mtandao.
Pia Bw. Muhidini Shaibu aliendelea kusema Tasaf inaendelea kuhakikisha inatoa Elimu ya namna ya kutumia pesa ya Tasaf inayotolewa kwa Walengwa ili watumie pesa hizo kwa kujikwamua kiuchumi na sio kwa matumizi mengineyo ambayo hayatakuwa na tija kwa kaya husika.
Uibuaji wa miradi mratibu wa Tasaf Wilaya alisema Zoezi la uibuaji miradi ya Tasaf linandelea na kuendelea na mpango wa PWP katika vijiji vipya vilivyo ingia kwenye Mpango wa Tasaf kwahiyo amewataka Walengwa kufuata taratibu za Tasaf kama zinavyo taka ili kufikia malengo
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.