Milioni 194 kunufaisha vijana na wanawake
Jumla ya shilingi milioni 194 zimetolewa na halmashauri ya tunduru kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake na vijana na walemavu 94 vilivyokindi vigezo na kufuata taratibu za mkopo.
Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi kaimu Mkurugenzi Mtendaji wilaya ndg Chiza Marando amesema wanakumbana na changamoto ya kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya wanavikundi,kutofuata katiba walizojiwekea, na migogoro baina yao inayopelekea vikundi kuvunjika na kushindwa kurejesha mkopo kwa Halmashauri.
kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru ndg Chiza Marando alisema mikopo hii ni endelefu hivyo ni vyema kwa kila kikundi kurudisha kwa wakati fedha walizokopeshwa ili na wananchi wengine waweze kupata mkopo.
Akiwahutubia wananchi baada ya kukabidhi Hundi ya Milioni 194 kwa vikundi vya wanawake, walemavu na vijana vipatavyo 94 vilivyopata mkopo leo, mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera alisema fedha hizi muwekeze katika biashara na zitumike kwa kazi mliyoombea ili ziweze kuzalisha na kuwasaidia kuondokana na hali ngumu ya maisha.
Pia ameupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru kwa kutenga fedha za asilimia kumi na kuwezesha vikundi vya wanawake, Vijana na walemavu ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapunduzi (CCM)ya mwaka 2015 hadi 2020.
Pia aliendelea kusema kuwa nawakumbusha wananchi kurudisha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwezesha na wengine kukopa na Halmashauri kuwa na uwezo wa kukopesha vikundi vingi zaidi.
"nasema wale watakaorudisha fedha hizi kwa wakati ndio serikali itawakopesha tena kwa awamu nyingine tena na watakaoshindwa kurejesha hatutasita kuwachukulia hatua za kisheria"
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduru mh Mbwana Mkwanda Sudi aliwataka wanaume kutoingilia matumizi ya fedha za mkopo waliochukua wanawake ili waweze kuendeleza shughuli zao na kujikwamua na umaskini.
"niwaombe wanaume wenzangu kuacha kuchukua fedha hizo na kudai gawio kutoka kwa wake zetu na wengine kuchukua na kwenda kuongeza familia ya pili"
Lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanakua na hali nzuri za kiuchumi na kujikwamua na umaskini, hivyo tushikiane kwa pamoja katika kuleta maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.