Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mh.Hairu Mussa alisema “Hali ya ukusanyaji Mapato sio zuri sana kwa sasa katika robo hii ya pili kwa Mapato ya Ndani tumeweza kupata TZS 1,645,526,894.38 amabapo kutoka Julai hadi December Halmshauri imeweza kukusanya Jumla ya Mapato ni Tzs 2,553,034,258.57 Sawa na 54% ya lengo la Mwaka kwahiyo Waheshimiwa Madiwani kwa Kushirikiana na Wataalam tuhakikishe tunaendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia kikamilifu vyanzo vilivyopo ili kufikia Malengo ya mwaka”.
Kwa upande wa Idara ya Afya Mh.Hairu Mussa aliseama “kwanza naomba nitoe pongezi zangu za dhati kwa Kamati ya Elimu,Afya na Maji, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ,Mganga Mkuu wa Wilaya na Timu yake yote ya wataalam wa Afya kwa kuweza kuisimamia idara ya Afya na kuleta nidhamu kwa Watumishi wetu wa Afya”.
Pia Mwenyekiti wa Halmashauri alitoa Shukurani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT.SAMIA SULUHU HASSANI Kwa kuipatia Idara ya Afya 1,100,000,000/=, Kwajili ya miradi ya Ukarabati wa Hospitali ya Wilaya,Ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Likweso, Ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Namasalau, Ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Malombe na Ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Nangolombe”.
Mh.Hairu Mussa aliendelea kusema “Pia ikumbukwe Kupitia Mapato ya Ndani Halmashauri imetenga 343,523,169.67 kwajili ya kumalizia Miradi ya Afya kama ifutayo :- Kituo cha Afya Nakayaya, Nalasi, Masonya ,Zahanati ya kijiji cha Angalia na Zahanati ya Kijiji cha Mnazimmoja lengo vikamilike na Wananchi wetu waanze kupata Huduma”.
Pia Mh.Mwenyekiti aliwakumbusha Wananchi na Vingozi wote kuwa katika swala la Afya zetu tukumbuke kuwa UKIMWI upo kwahiyo ni vizuri tuchukue hatua ikiwemo matumizi ya Kondomo pia ni vema kwa sisi Viongozi hii iwe ajenda yetu ya Kudumu katika Vikao vyetu Mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.