Ndg. Gasper Zahoro Balyomi (kushoto) ambae ni mkurugenzi aliemaliza muda wake wa kufanya kazi katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru, akimkabidhi ofisi Ndg. Chiza C Marando (kulia) ambae ni mkurugenzi mpya katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru.
Ndg. Gasper Zahoro Balyomi alitoa taarifa fupi kuusiana na idara mbali mbali zilizopo ndani ya halmashauri, kama vile idara ya elimu katika ngazi ya elimu msingi halmashauri inaendeleza ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama vile vyoo na madarasa pia ngazi ya elimu sekondari inaendeleza ujenzi wa mahabara za shule.
Pia Ndg. Gasper Zahoro Balyomi alikiipongeza kitengo cha Tehama kwakuweza kuweka utaratibu wa kila baada ya wiki mbili au mwisho wa mwezi kuangalia wadaiwa (defaulters), ambayo inamsaidia mkurugenzi kuwabana wadaiwa walipe madeni yao.
Ndg.Chiza C Malando Mkurugenzi wa sasa wa halmashauri wilaya ya Tunduru alitoa shukrani za dhati kwa Ndug.Gasper Zohoro Balyomi na watumishi wote waliohudhuria kikao hicho, pia alimuomba afisa utumishi kupanga siku ya kikao kitachohusisha wakuu wa idara wote ili kuweza kuijenga halmashauri ya wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.