Mahadhimisho hayo katika wilaya ya Tunduru yamefanyika kwa kushirikisha wanafunzi wa kike na wa kiume kutoka shule mbalimbali katika wilaya ya Tunduru ,katika hafla hiyo ya mahadhimisho hayo ndugu ASIA LUGOME katibu talafa wa talafa ya nakapanya wilayani Tunduru alizungumza na watoto wa kike kuhusiana na masuala mbalimbali yawahusuyo wanawake.
Mgeni rasmi kwanza aliwapongeza watoto wa kike katika kijiji cha namasakata shule ya sekondari namasakata kwa ubunifu wao wa kushona taulo za kike kwa malighafi za kawaida(home made ),mgeni rasmi pia alisisitiza kumsikiliza motto wa kike na kumshirikisha katika maamuzi
Mgeni rasmi aliwataka ustawi wa wajamii na wadau mbalimbali wanaohusika na kujenga jamii kutoa elimu ya kujitambua kwa mtoto wa kike ili awezi kupamabana na changamoto anazokutana nazo katika jamii na pia kupunguza vitendo vya unyanyasaji kwa mtoto wa kike na jamii kwa ujumla
Pia amewataka watoto wa kike na jamii kwa ujumla kutoa taarifa za vitendo viovu vinavyoendelea katika jamii na kudumusha ushirikiano baina ya wanawake wenyewe na wanaume pia,wakiwa na kauli mbiu isemayo
“HAKI ZETU NI HATIMA YETU WAKATI NI SASA”
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.