Hayo yamesemwa na kamati ya ufuatiliaji inayofanya ukaguzi wa utendaji kazi wa maafisa habari/ Mawasiliano katika taasisi mbalimbali za serikali, kufuatia maagizo yaliyotolewa katika mkutano wa 14 wa maafisa habari na mawasiliano serikalini ulifanyika jijini Arusha mwezi machi 2018 ya kuwataka chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO) kushirikiana na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kufanya ziara ya katika ofisi za maafisa mawasiliano ili kuchochea utendaji kazi wao.
Akiwasilisha ujumbe huo katika ofisi ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kiongozi wa msafara kutoka Ofisi ya Msemaji mkuu wa serikali Ndg Casmiri Ndambalilo alisema kazi kubwa ya maafisa mawasiliano ni kuisemea serikali inavyotekeleza majukumu na kuleta uwazi kwa wananchi inayowahudumia.
Aidha alisema ili waweze kutekeleza majukumu ya mawasiliano ya kimkakati kuisemea serikali ipasavyo, halmashauri inatakiwa kuwawezesha vitendea kazi, kuwashirikisha katika vikao vya maamuzi na kupewa rasimali za kuitembelea miradi inayotekelezwa ndani ya taasisi zao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg Chiza Cyprian Marando aliwapongeza kufika kufanya ufuatiliaji kwani serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh.John Pombe Magufuli inahitaji ukweli na uwazi na ili wananchi waweze kujua serikali yao inafanya nini ni lazima kutoa taarifa za mara kwa mara kwa wananchi kupitia vyombo vya Habari.
Ndg Chiza Marando alisema “ halmashauri ya Tunduru haikuwa na Afisa Habari kwa kipindi kirefu sana, na mtu muhimu sana ambaye tulitamani kuwa naye na toka alipofika tumejitahidi kupamtia vitendea kazi, na kumshirikisha vikao vyote vya maamuzi, na hata kwenye ukaguzi wa miradi anashirikishwa vizuri , hivyo anaifahamu halmashauri vizuri.”
Hata hivyo walimpongeza Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Tunduru kwa kutambua umuhimu wa Afisa Mawasilaino katika taasisi yake na kutekeleza kwa wakati maagizo yaliyotolewa na viongozi ikiwa ni pamoja na kununua vitendea kazi kwa ajili ya Ofisi ya Habari, Ushirikishwaji wa Afisa Habari katika vikao vya maamuzi.
pamoja na pongezi hizo Kamati ya Ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Msemaji Mkuu wa serikali na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini walimtaka Afisa Habari kutumia fursa aliyoanayo kutoa taarifa mbalimbali za halmashauri yake kupitia Idara ya Habari maelezo ajili ya kutangaza katika vyombo vya Habari.
Imtolewa na
Theresia Mallya
Afisa Habari Halmashauri.
25/07/2018
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.