Tume ya Utumishi wa Walimu Rudisheni Maadili ya Walimu.Dkt Ndumbaro.
Hayo yamesemwa katika kikao cha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt Laurean Ndambaro akiwa katika ziara ya kuwakumbusha watumshi wa umma muelekeo wa serikali ya awamu ya tano katika kujenga misingi ya utumishi wa umma.
Aidha alisema serikali inatarajia kuwa na watumishi wenye uadilifu uliotukuta katika jamii na utoaji huduma kwa wananchi, watumishi wanaowajibika kwa serikali nawananchi, nidhamu ya kazi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, ndio dira ya serikali na itasimamia kuona kuwa utekelezaji unafanyika.
Dkt. Ndumbaro alisema kufuatia kuwepo na malalamiko mengi katika ofisi yake anaugiza uongozi wa tume ya kusimamia maadili ya walimu Nchini TSC kuhakikisha kwamba nidhamu ya walimu inarudi na kada hiyo kuheshimika kama ilivyokuwa hapo awali.
Dkt. amesema watumishi wanatakiwa kufuata sheria , kanuni na Taratibu za Umma na kuacha kuiabisha serikali kwa kuchukua mikopo iliyopitiliza kwani serikali imeweka sheria ya mtumishi kukopa isiwe zaidi ya 1/3 ya mshahara wake anaopokea ili aweze kumudu maisha na kuendelea kutekeleza majukumu yake.
“kumukuwa na tabia ya walimu kukopa kupitiliza hata baada ya serikali kuweka sheria ya kiwango cha kukopa kisizidi 1/3 ya mshahara anaopokea wameamua kuhamia katika makampuni yanayokopesha fedha na kupeleka hadi vitambulisho vya benki na nyaraka nyingine kwa udhamini, hali hii inadhoofisha uwajibikaji na kuharibu nidhamu ya kazi”
Aidha dkt. Ndumbaro ameigaiza tume ya kushughulikia maadili ya walimu nchini TSC kushghilikia masuala ya walimu kikamilifu na kuacha kuingiza siasa katika kazi na kama mtumishi amefanya kosa basi aadhibiwe kulingana na kosa alilofanya. “niwaombe makatibu wa TSC nchini kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa na serikali katika kushughulikia kesi za walimu”
Dk Ndumbaro aliendelea kusema kuwa ni jukumu la kila mkuu wa Idara na kitengo kusimamia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma ili kuweza kuleta maendeleo chanya kwa watu anawasimamia na kuondoa kero na malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara kwani kuna matatizo mengine ni madogo ambayo yako ndani ya uwezo wa mkuu wa idara au kitengo kuweza kuyatatua.
Aidha dk Ndumbaro alisema ni vyema Halmashauri kujiwekea utaratibu wa kuwapongeza watumishi wanaotimiza wajibu wao vizuri ili kuongeza morali ya utendaji kazi kwa watumishi na kwa wale wanaokiuka maadili ya utumishi na kuwa wazembe katika kazi kupewa onyo kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa Umma.
Dkt.Ndumbaro alisema suala la uhamisho kwa watumishi kutoka katika kituo kimoja cha kazi kwenda kingine wa lipo ndani ya uwezo wa mkuu wa taasisi na hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuzuia uhamisho huo baada ya mtumishi kukidhi vigezo vyote muhimu na kama mtumishi huyo yupo mmoja mkuu wa taasisi anatakiwa kutoa maoni ya kupewa mtumishi mwingine na sio kuzuia uhamisho.
“nimekuwa nikipokea malalamiko mengi katika ofisi yangu kuhusu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara na vitengo kuwazuia baadhi ya watumishi kuhama kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kingine, hii haki ya mtumishi na ni wajibu wa serikali vilevile kumpelaka mtumishi mwingine kwenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi”dkt ndumbaro alisisitiza
Watumishi wa Umma waliopo katika wilaya ya Tunduru wakimsikiliza katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Utumishi wa Umma Dkt.Laurean Ndumbaro katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa skyway Tunduru tarehe 10/11/2017.
Dkt. Alisema katika kipindi cha mwezi novemba sekrikali italipa madeni ya mishahara ya watumishi, kupandisha vyeo na madaja na ongezeko la mshahara kwa watumishi wote wa umma waliofikia vigezo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera alimshukuru katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kufanya ziara katika wilaya ya Tunduru na kuweza kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo watumishi katika kutekeleza majukumu yao ya kila katika maeneo yao ya kazi.
Mkuu wa wilaya Homera alisema kuwa Tunduru ina upungufu mkubwa wa watumishi hasa katika sekta ya Afya ambayo kuna mganga mmoja tuu huku wakiwa na mahitaji ya waganga 28 ili kuweza kutoa huduma, na kuna baadhi ya zahanati hazina kabisa watumishi na zilifungwa kwa muda kutokana na uhaba wa watumishi katika idara ya afya.
“tunaomba wilaya ya Tunduru iangaliwe kwa jicho la pili katika ikama ya watumishi kwani kuna upungufu mkubwa sana ukilinganisha idadi ya watumishi na ukubwa wa eneo la kiutendaji na huduma zinazohitajika kwa jamii”
Hata hivyo katika shule zetu kuna upungufu mkubwa wa walimu ambapo unakuta kuna baadhi ya kuna walimu wawili hadi watano ndio wanafundisha kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba, hali hii inapekelea kiwango cha ufaulu kushuka na mwalimu kuwa mzigo mzito sana alisema Mkuu wa wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera akifungua kikao na kumkaribisha katimu mkuu ofisi ya Rais Utumish wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro kuongea na watumishi wa wanahudumu katika wilaya hiyo
Alimalizia kwa kuwapongeza watumishi wa Halmashauri ya Tunduru kwa uwajibakaji na utendaji wao kazi uliotukuka na kuwataka kuendelea na moyo huo huo wa kuwatumikia wananchi wa Tunduru ili kuweza kuleta maendeleo kwa wananchi kuloingana na sekta zao.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.