Maadhimisho ya siku ya familia dunia kila mwezi wa tano tarehe 15 kila mwaka ,wilaya ya Tunduru imeungana na wanafamilia wote kote dunia kuadhimisha siku hiyo.
Katika maadhimisho hayo wilayani Tunduru yamefanyika katika kata ya majengo katika shule ya msingi muungano na Mgeni rasmi alikuwa mheshimiwa diwani wa kata hiyo mh.Abdallah Rajabu Abdallah , katika maadhimisho hayo yaliudhuliwa na ofisi ya ustawi wa jamii ,dawati la jinsia na ofisi ya upingaji ukatili wilaya ya Tunduru (SMAUJATA).
Wanafamilia walisisitizwa suala la kudumisha upendo pamoja na kuyatunza maadili mema hasa kwa watoto wa kizazi hiki na manufaa ya kizazi cha baadae,pia kupitia mwenyekiti wa kampeni huru yaupingaji ukatili SMAUJATA ndug. FLorian Mrope amewasisitiza wanafamilia katika upingaji wa aina yeyote ya ukatili ambao unafanyika katika maisha yetu ya kila siku pia kupitia dawati la kijinsia la Tunduru limewataka wananchi na wanafamilia kwa ujumla kuripoti mambo yote maovu yanayofanyika katika jamii zetu ili kujenga familia bora na yenye maadili mema kwa kizazi cha sasa na kijacho yalisemwa na afande wa dawati la jinsia WP 7391 CPI Asia Botea.
Afisa ustawi wa jamii wilaya Bi Blandina Sekula ameiomba jamii hasa wazazi kuwa na ukaribu na watoto kwa kuwa utimilifu wa familia ni pamoja na watoto , kwahiyo ametoa rai kwa wazazi wote ulimwenguni kuwa na utaratibu wa kutenga muda kwaajili ya kuketi na watoto pamoja ili kujua changamoto zao katika jamii waishiyo na kuweza kufahamu mahitaji ya karibu ya watoto wao.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.