Tunduru 30, Oktoba 2019.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma inapenda kukanusha habari ya upotoshaji iliyotolewa na Gazeti la Habari Leo la tarehe 28 Oktoba 2019 na Kituo cha Televisheni cha ITV ikisomeka kuwa “Wanafunzi 350 waacha shule kwa utoro, mimba,” habari hii haina ukweli wowote kama ilivyoripotiwa.
Tunapenda kuuarifu umma kuwa baada ya kuwepo kwa taarifa hiyo Ofisi ya Mkurugenzi imefanya ufuatiliaji wa kina katika Shule ya Sekondari Marumba ambayo imetajwa katika habari hiyo iliyosema kuwa wanafunzi 350 wa shule hiyo wameshindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya utoro na mimba kwa kipindi cha miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2016 hadi 2019.
Ni vyema umma ukafahamu kuwa katika kipindi cha miaka minne yaani 2016 hadi 2019, shule hii ilipangiwa idadi ya wanafunzi 603 ikiwa wavulana 320 na wasichana 283, waliosajiliwa kwa kipindi hicho ni wanafunzi 515 ikiwa pungufu ya wanafunzi 88 kati ya waliopangwa.
Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanafunzi waliopo katika shule ya Sekondari Marumba hadi kufikia tarehe 28/10/2019 ni 345 ikiwa wavulana 208 na wasichana 137 kukiwa na upungufu wa wanafunzi 170.
Akitoa ufafanuzi huo Mkurugenzi Mtendaji Halmasahuri ya Tunduru Gasper Balyomi amesema hii ni wazi kuwa idadi ya wanafunzi 350 wa sekondari ya Marumba walioripotiwa hawajulikani walipo hazina ukweli wowote kufuatia takwimu zilizotolewa na kubaini kuwa:-
Hivyo kufanya jumla ya wanafunzi 170 kwa kipindi cha miaka minne ndio hawapo shuleni tofauti na taarifa ilivyoonesha jumla ya wanafunzi 350 wa shule hiyo wameacha masomo.
Aidha kuhusu suala la utoro wa reja reja Halmshauri inaendelea kushirikiana na wazazi pamoja walezi wa wanafunzi katika kuahikisha utoro mashuleni unadhibitiwa.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Tunduru
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.