Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,Mhe. Simon Chacha ameshuhudia zoezi la utiaji wa saini kwa Askari wa Uhifadhi wa Kijiji (VGS) 20, ambao wataenda kufanya kazi ya ulinzi wa maeneo ya jumuiya za wanyamapori za Chingoli na Nalika.
kikao hicho cha utiaji saini kimehudhuriwa pia na Katibu tawala wa Wilaya Ndg. Milongo Sanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Tunduru Ndg. Chiza Marando, Kaimu Afisa maliasili wa Wilaya, Meneja wa miradi Nyanda za juu kusini-Honey guide, Wenyeviti wa bodi ya wadhamini wa jumuiya zote mbili na Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Mpaka sasa Wilaya ya Tunduru ina jumla ya Askari wa Uhifadhi wa Kijiji (VGS) 210.
Juhudi hizi zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Uhifadhi wa kuwapatia mafunzo Askari ambao watakuwepo maeneo ya vijiji, ni kuhakikisha inaondoa migongano kati ya Binadamu na Wanyama.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.