Jumla ya shilingi milioni 11 zimetolewa na kiwanda cha kubangua korosho cha Korosho afrika kilichopo katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kuchangia ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Nakakaya, kituo hiki cha afya kinajengwa kwa mchango wa serikali na mchango wa wafanyabisha wa wilayani Tunduru.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Nakayaya kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassimu Majaliwa Mb, alipotembelea kukagua ujenzi wa kituo hicho , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wilaya Ndg Chiza C Marando alisema kuwa mradi huu umeibuliwa na mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera mwaka jana na utatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 1.6 hadi kukamilika.
Na mpaka hapa kilipofikia ni mchango kutokana na wafanyabiasha waliopo katika wilaya ya Tunduru na wadau wengine wa maendeleo ndio waliotoa michango yao ya mchanga, vifaa vya kiwandani na fedha taslimu baada ya mkuu wa wilaya kuwashikisha wameonesha muamko wa uchangiaji.
Waziri Mkuu afanya ukaguzi wa kituo cha Afya Nakayaya
Akiongea na watumishi, viongozi na wananchi wa kata ya Nakayaya baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kaasimu Majaliwa amesema kutokana na ongezeko la watu katika wilaya ya Tunduru huduma za afya zinatakiwa kupanuliwa, hivyo nawapongeza viongozi wa wilaya kwa kuanza kutekeleza miradi yenye tija kwa wananchi.
Waziri mkuu amesema nimesikia katika taarifa ya wilaya kuwa hospitali ya wilaya imelemewa na wagonjwa kutokana onegezeko la watu, pia kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa barabara katika kiwango cha lami kumesababisha kuwa na ongezeko kubwa la magari hivyo ni vyema kupanua huduma za afya pia.
Waziri mkuu Kassimu Majaliwa alisema viongozi wa wilaya waendelee kuwashikirisha wananchi hata wa kawaida kuchangia ujenzi wa kituo hicho ili kiweze kukamilika kwa wakati na serikali kupitia wizara ya afya italeta wataalam wa kutoa huduma katika kituo hicho mara kitakapokamilika.
“Serikali imeweka kipaumbele katika kuwahudumia wananchi na katika ilani ya chama cha mapinduzi imepanga kila kata kuwa na kituo cha afya lakini pia kila kijiji kujenga zahanati katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi”alisema waziri mkuu.
kaimu Mkurugenzi chiza Marando Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo cha afya Nakayaya kwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassimu Majaliwa wakati akiwa ziarani wilayani Tunduru
Akipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 11 iliyotolewa na kiwanda cha kubangua korosho Tunduru cha Korosho Afrika kwa ajili ya kuchangia uendelezaji wa ujenzi waziri mkuu Kassimu Majaliwa aliushukuru uongozi wa kiwanda hicho kwa kuchangia huduma za jamii katika wilaya ya Tunduru.
pia aliwashurukuru wabunge wa wilaya ya Tunduru kwa kumuunga mkono katika kuchangia ujenzi wa kituo hicho ambapo jumla ya shiling milioni 32, bati 50 na mifuko ya saruji 150 viliadiwa na wabunge wa Tunduru Kaskazini Eng Ramo Makani, Tunduru Kusini Mh Daimu Mpakate na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Mh Sikudhani Chikambo pamoja na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme.
Waziri mkuu Kassimu Majaliwa alisema serikali inaendelea kuimarisha huduma za afya na wilaya ya Tunduru ipo katika mpango wa uboreshaji wa vituo vya afya vya Mkasale na Matemanga ambavyo vimetengewa bilioni moja, yaani milioni 500 kwa kila kituo cha afya za kuboresha majengo ya kutolea huduma.
waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionesha hundi ya m
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.