Katika kuazimisha siku ya wajane duniani ,leo Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kupitia idara ya maendeleo ya jamii imeshiriki maadhimisho hayo kwa kukutana na wajane wa wilaya ya Tunduru na kutoa elimu na kujadili masuala mbalimbali yawahusu wajane, katika kata ya Nanjoka ,kijiji cha Nanjoka na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Mheshimiwa Diwani wa kata hiyo Saidi Kihosa.
Katika maadhimisho hayo pia wadau mbalimbali walishiriki wakiwemo wadau wa sheria, ustawi wa jamii na wanadawati la jinsia.
Ambapo mada mbalimbali zilijadiliwa na elimu juu ya haki na wajibu wa wajane kisheria zilitolewa.
Katika muendelezo wa majadiliano hayo na elimu. Hakimu mkazi, mahakama ya mwanzo tarafa ya Nakapanya Bi jane pascal Mudogo alieleza juu ya haki ,wajibu na taratibu za kisheria juu ya urithi wa mali zilizoachwa na wenza wao, aliwaambia wanatakiwa kufuata taratibu zote za kisheria ikiwa pamoja na kufika mahakamani ili kupata msaada wa kisheria katika masuala hayo.
Pia Bi jane aliwasihi wajane kutoshikamana au kukubaliana na mila na desturi za kurithiwa baada tu ya mwenza wao kufariki , aliwataka kushirikiana na vyombo vya dola katika kutokomeza milana desturi hii kwan ni kosa kisheria kufanya hivyoo.
Aidha Bi Brandina Sekela afisa ustawi wa jamii (W) Tunduru aliwaomba wajane kuwa wabunifu na kutafuta fursa mbali mbali ili kuweza kupambana na kuzidi kujiinua kiuchumi kwa sababu kuondokewa na wenza sio mwisho wa maisha yatubidi kupambana ili kuweza kushindana na hali ya maisha ya kila siku, alisema.
Kwa upande mwingine Mhe.Diwani Saidi kihosa alizungumza kwa kuanza kuwapa polee wajane kwa wakati mgumu waliopitia na wanaoendelea kuupitia ,pia aliwatia imani na nguvu kuwa bado wana nafasi ya kuendelea katika kuboresha familia zao na kusimami mlezi ya watoto wao, kwa muktadha huo aliwataka wajane kudumusha upendo kuwasimamia watoto wao katika maadili yanayopaswa na stahiki ili tuweze kuwa na kizazi bora cha hapo baadae.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.