Madiwani wa Halmashsuri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wameipongeza Serikali Kwa kuipatia fedha Nyingi zilizo iwezesha Halmashauri yao kutekeleza Miradi mingi
Hayo yalibainishwa katika kikao cha cha baraza la madiwani cha Robo ya pili ya mwaka 2022 kilicho fanyika katika ukumbi wa Klasta ya Walimu wa Baraza la Mlingozi mjini hapa na kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja jumla ya shilingi Bilioni 2.110 zimeletwa na serikali.
Alisema katika kipindi hicho halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni1.410 kwa ajili ya Ujenzi wa shule tatu mpya za sekondari katika Kata za nakayaya, Lukumbule na majimaji.
Alisema sambamba na fedha hizo pia katika kipindi hicho jumla ya shilingi milioni 700 zilizo tumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya vituo vya afya 2 na zahanati 4 zikiwa ni juhudi za serikali kusogeza huduma kwa jamii.
Aidha Mh.Hairu Hemedi Mussa pia akatumia nafasi hiyo kuwapongeza viongozi wa Halmashauri hiyo kwa ushirikiano walioufanya kipindi cha mapokezi ya mwenge wa uhuru zilizofanyika April 15-16/ mwaka huu ambapo hakuna mradi ulio kataliwa.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Tunduru Mwl. Mohammed Mavala pamoja na mambo mengine alisema kuwa pamoja kutokuwepo kwa miradi ya mwenge iliyokataliwa lakini zipo dosari ambazo zimekuwa zikijitokeza katika ujenzi wa miradi ya serikali.
Aidha katika taarifa Mavala akamtaka mwenyekiti wa Halmashauri kuhakikisha kila idara zote katika Halmashsuri yake zinakuwa na vitabu vya Irani ya chama ili kuwa na Dira ya utekelezaji wa Miradi yake ili kuwa na uhakika wa miradi yote iliyo ainishwa kwenye irani hiyo ili itakapo fikia kipindi kilicho pangwa ikamilike kwa wakati.
Katika taarifa hiyo Katibu akatumia nafasi hiyo kuwaagiza Wataalamu kuzingatia utoaji wa ajira za watu watakao tumika katika shughuli za uandikishaji wa zoezi la Sensa ya watu na makazi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Tunduru Mustafa Bora
Akatumia nafasi hiyo kuwataka Wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na makazi inayo tarajiwa kufanyika Agost 23 Mwaka huu.
Awali Mratibu wa sensa ya watu na makazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Enock Kabakaki alisema kuwa tayari zoezi hilo limepangwa kufanyika kidijitali lipo tayali kupitia ofisi ya Takwimu za Taifa imeandaa Madodoso 4 ya msingi kwa jamii, majengo au nyumba na makazi zitakazo tumika kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Kabakaki aliendelea kufafanua kuwa hadi sasa tayari wameanza kubainisha na kutenga maeneo 1,176 ambayo yatatumika kwa ajili ya kuhesabiwa pamoja na kuunda kamati za wilaya, Vijiji , vitongoji na kwamba pia hadi sasa zoezi la usajili wa anuani za makazi limefanywa kwa asilimia 102.
Akitoa salamu za serikali kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius mtatiro , kaimu afisa tawala wa Wilaya Augustino Maneno pamoja na mambo mengine aliwataka madiwani kuendelea kutoa elimu na maelekezo ya namna zoezi hilo la sensa litakavyofanikiwa.
“Wote tunajua kilicho jitokeza katika awamu ya sensa iliyopita hivyo kila kiongozi inafaa ajipange na kulifanya zoezi hilo kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyetu” alisisitiza Maneno na kuongeza kuwa hiyo iwe chachu ya mabadiliko katika jamii yetu ili kufikia malengo.
Sambamba na maelekezo hayo pia akatumia nafasi hiyo kwa kuwataka madiwani hao kuwaelekeza wananchi wao juu ya utekelezaji wa zoezi la uwekaji wa anuani za makazi katika makazi yao lililopo mbele yao.
Aidha maneno pia aliwataka wanafamilia kutunza chakula baada ya msimu wa mavuno ili kujiondoa kwenye adha ya upungufu wa chakula endapo unaweza kutokea mbeleni.
Kuhusu utekelezaji wa miradi inayo tolewa na Serikali ikiwemo ya ujenzi wa miradi ya ujenzi wa shule za Sekondari na Vituo vya Afya katika kata za Majimaji, Lukubule na Nakayaya kuwa imekuwa ina kusuasua sana utekekezaji wake hasa kwenye upande wa nguvu za wanachi hali inayo onesha kuto kuwepo kwa maelekezo ya kutosha kwa viongozi wao.
Akitoa neno la shukurani Makamu mwenyekiti wa Halmashsuri ya Wilaya ya Tunduru Said Bwanali pamoja namambo mengine alisema madiwani wameyapokea maelekezo yote na kuahidi kuyafanyia kazi katika kipindi chao chote cha uwakirishi wao kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.