Katika baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Tunduru lililofanyika katika ukumbi wa klasta ya Mlingoti waapishwa madiwani wa Kata za Kalulu na Lukumbule.
Akifungua mkutano wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2017/2018 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduru Mh mbwana mkwanda Sudi alianza kwa kuwapongeza madiwani waliochaguliwa wa Kata za Kalulu na Lukumbule kwa kushinda nafasi hizo na kuwakaribisha rasmi katika baraza la madiwani.
Mkwanda Sudi aliendelea kusema kuwa ni vyema madiwani na wananchi wakashirikiana pamoja na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayopelekwa katika maeneo yao ya utawala ili kuleta ufanisi na matokeo Chantal kwa jamii.
Wataalam wa Kilimo niwaombe muwasaidie wananchi katika Kata zenu ili waweze kufanya kilimo chenye tija na kuongeza uzalishaji kwa ukuzaji wa uchumi wa Tunduru na mtu mmoja mmoja. Alisema mwenyekiti wa Halmashauri.
Nasisitiza katika dhana ya utawala bora,utunzaji wa siri, ukweli na uwazi ili kuondoa migogoro inayaoweza sababishwa na kukosa uadilifu miongoni mwa viongozi na watendaji.
Ninaomba tusimamie Elimu na tuhakikishe kuwa Watoto waliofaulu Katika maeneo yetu ya uongozi wanaripoti shule kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.