KAMPENI ya Utunzaji Mazingira Yapata Kasi Wilayani Tunduru.
Shirika la Uhifadhi wa Mazingira na Maliasili Duniani (WWF),limeendesha kampeni ya saa moja la utunzaji wa mazingira (60 Earth Hour) katika, Kata ya Sisi kwa Sisi, Kijiji cha Sisi kwa Sisi Katika Shule ya Msingi Mahauhau Wilayani Tunduru.
Kupitia kampeni hii ya saa moja iliyotolewa kwa upandaji wa miti imekuwa ishara na azma ya kuendeleza jitihada za kutunza mazingira, ambayo ni sehemu ya kampeni ya Utunzaji Mazingira Duniani inayofanyika kila mwaka ifikapo Machi 23.
Akizungumza baada ya zoezi la upandaji miti, Ndg. Deogratius Kilasara, Afisa Uhifadhi kutoka WWF, ameeleza kuwa lengo kuu la zoezi hili ni kuhamasisha utunzaji wa mazingira. Amesisisitiza kuwa jitihada za kutunza mazingira zinapaswa kuwa endelevu na ni jukumu la kila mmoja katika jamii.
“Tuondokane na zana ya kuwa, utunzaji wa Mazingira ni wa kundi Fulani pekee, bali tujjue kuwa kutunza mazingira ni jukumu la kila mmoja katika Jamii”. Alisema Kilasara.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mahauhau, Bi. Rozina Ngonyani, ameeleza mikakati yao ya kuhakikisha wanatunza mazingira kwa uangalifu, ikiwa ni pamoja na kuendelea kufuatilia ukuaji wa miti ili kuhakikisha manufaa yake yanadumu.
Kwa upande wake, Faraja Mussa, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mahauhau, ameishukuru WWF kwa kuwawezesha kushiriki katika jitihada za utunzaji wa mazingira na ameahidi kuchukua jukumu hilo kwa uzito, akiahidi kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha na kusaidia jamii katika utunzaji wa mazingira.
Kaimu Afisa Maliasili na Hifadhi za Mazingira, Ndg. Dunia Almasi, ameishukuru WWF kwa ushirikiano wao katika jitihada za kutunza mazingira. Amesema mazingira ni nyenzo muhimu katika uhai wa binadamu na ametoa wito kwa jamii kushirikiana katika kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kampeni hii imeleta matumaini mapya kwa jamii ya Sisi kwa Sisi na imeonyesha umuhimu wa ushirikiano katika kudumisha mazingira safi na endelevu.
Kampeni Hiyo imeenda sambamba na Kauli mbiu isemayo #Earth hour BiggestHourForEarth
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.