Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani Tunduru, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Shule mpya,Majengo ya Tehama, Maktaba,Mabweni na Matundu ya Vyoo.
Pichani:Muonekano wa Jengo la Bweni katika Shule ya Sekondari ya Tunduru.
Pichani:Muonekano wa Maabara Iliyojengwa katika Shule ya Sekondari Kungu
Kamati huangalia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uwiano wa gharama na kazi iliyofanyika, ubora wa vifaa na kazi Zilizofanywa, muda wa utekelezaji wa mradi na matumizi sahihi ya fedha za mradi.
Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mhe. Hairu Hemed Musa, na iliambatana na waheshimiwa Madiwani ambao ni wajumbe wa kamati hiyo pamoja na Wataalamu mbalimbali toka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya.
Aidha, Kamati hiyo imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo na kuagiza kuwa miradi yote ikamilike na kukabidhiwa ifikapo Januari 28,2024.
Ukaguzi huu wa miradi wa mara kwa mara unasaidia kutambua mapungufu yoyote katika utekelezaji wa miradi, na hatua za kurekebisha mapungufu hayo huchukuliwa mara moja.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.