Kaimu mkurugenzi Mwl Andrea Mwalongo amewata wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru wachangamkie fursa zinazo tarajiwa kuletwa na Bank ya NBC ambayo bank hiyo inatarajia kufungua tawi lake hapa Tunduru hivi karibuni amesema hayo katika mkutano wa tamcutunduru ulio dhaminiwa na NBC bank
Pia bank ya NBC yenyewe imejipaga kutoa mikopo kwa wakulima wa korosho,kahawa,tumbaku,ufuta na mpunga kwa kauli mbiu ya NBC Shambani hivyo mara baada ya kufunguliwa tawi la NBC siku za hivi karibuni wananchi wa Tunduru wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zitatolewa na NBC bank katika Halmashauli ya Wilaya ya Tunduru
Aidha Mwenyekiti wa tamcutunduru Ndg Hashimu Twaribu Mbarabara wakati akifungua mkutano kabla hajamkaribisha mgeni rasmi kaimu mkurugenzi nae amesisitiza wananchi wa Tunduru wachangamkie fursa ambayo inayo tarajiwa kuletwa na NBC
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.