Jukwaa la Wanawake Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma limezinduliwa tarehe 21 September 2023 likiwa na lengo la kuwapa fursa na kuwapambania wanawake waweze kujiimarisha kiuchumi na kujikwamua na kipato duni.
Akihutubia Jukwaa hilo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro, alisema Jukwaa hili likiwezeshwa kikamilifu litakua msingi wa kutatua changamoto mbalimbali, kwasababu katika falsafa ya uchumi mwanamke ana uwezo mkubwa wa kutunza Fedha, ni vyema kuwepo na uchumi shirikishi ndani ya familia.
“Jukwaa hili halijazinduliwa kwa maamuzi ya mtu mmoja, uundwaji wake ni maagizo ya mikataba mbalimbali pamoja na sheria ambazo zinalinda maslahi ya mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali inapinga vikali ndoa za utotoni, Binti aachwe asome”. Alisema.
Pichani (Aliyesimama): Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh. Julius Mtatiro.
Kwa upande wake Katibu wa jukwaa la wanawake Mkoani Ruvuma Mwl. Neema Kajange alisema, Mama ni mlinzi mkubwa wa familia na ili kumfikia mwanamke wa chini kabisa Halmashauri zitenge kifungu kitakachosaidia kuwaunganisha na kushiriki katika majukwaa yanayohamasisha shughuli za uchumi na uzalishaji mali.
Pichani: Katibu wa Jukwaa la Wanawake Mkoani Ruvuma Mwl. Neema Kajange.
Aidha, Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Wilayani Tunduru Bi. Somoe Singizi amewasisitiza wanawake Wilayani humo kushirikiana katika kutokomeza mfumo dume katika familia, aliongezea kusema, Wanawake ni jeshi kubwa hivyo ni jukumu la kila mmoja wao kujituma na kufanya kazi kwa bidii.
Pichani: Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilayani Tunduru Bi. Somoe Singizi.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum linasimamia, kutoa miongozo ya uanzishaji na uendeshaji wa Jukwaa la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ikiwa ni jitihada za kuhakikisha kuwa mipango ya Serikali inalenga katika kumwezesha mwanamke kiuchumi ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo stahimilivu kwa wanawake wa Taifa kwa ujumla.
Pichani (kuli): Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Mtatiro akikagua bidhaa za maonesho.
Kauli mbiu ya Jukwaa la Wanawake Mwaka 2023 ni “Mfumo Dume katika familia ni hatari kwa uchumi wa Mwanamke”.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.