• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

HOTUBA YA WAZIRI MKUU - UZINDUZI WA MFUMO WA UANDAAJI MIPANGO NA BAJETI ZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

Imewekwa : September 8th, 2017

HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.) WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UZINDUZI WA MFUMO, KUPANGA MIPANGO, KUANDAA BAJETI NA KUTOLEA TAARIFA (PLANREP) NA MFUMO WA MALIPO NA KUTOA TAARIFA ZA FEDHA ZA VITUO VYA KUTOA HUDUMA TAREHE 05 SEPTEMBA, 2017 - DODOMA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Mhe. George Simbachawene, (Mb.);

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma - Mhe. Angela Kairuki, (Mb.);

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Mhe. Jenista Mhagama, (Mb.);

 

Waziri wa Fedha na Mipango - Mhe. Dkt. Philip Mpango, (Mb.);

 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Mhe. Ummy Mwalimu, (Mb.);

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia - Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, (Mb.);

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma - Mhe. Jordan Rugimbana;

 

Makatibu Wakuu mliopo;

Makatibu Tawala - Mkoa wa Dodoma na Manyara;

 

Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania - Bi. Inmi Patterson;

 

Mkurugenzi wa USAID Tanzania - Bw. Andrew Karas;

 

Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma - Dkt. Emmanuel Malangalila;

 

Kiongozi wa Mradi wa Kuimarisha Huduma za Afya - Prof. M. Meshack;

 

Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma;

 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma;

 

Mtendaji Mkuu - Wakala wa Mitandao;

 

Mkurugenzi Mkuu - Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali;

 

Wakurugenzi wa Wizara na Taasisi za Serikali mliopo;

 

Wakurugenzi wa Halmashauri mliokuwa hapa;

 

Wakufunzi na Wataalam wote;

 

Waandishi wa Habari;

 

Mabibi na Mabwana.

UTANGULIZI - SHUKRANI NA PONGEZI

Kipekee nimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kukutana mahali hapa na kushuhudia uzinduzi wa mifumo hii miwili ya kielektroniki ambayo imeandaliwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kupitia ufadhili wa Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Sekta ya Umma (Public Sector System Strengthens – PS3) unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani.

Pia, napenda kutumia nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa George Simbachawene, (Mb.) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kunialika Kuzindua Mifumo hii Miwili muhimu ya kuboresha upangaji Mipango na Bajeti Nchini.

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI amenieleza kwamba Wataalam wetu Serikalini kwa kushirikiana na wataalam wa PS3 walifanya kazi hii usiku na mchana kuhakikisha wanafanikiwa kutengeneza mifumo hii maalum ya kuandaa Mipango na Bajeti kwa ajili ya Mamlaka za Serikali za Mitaa “Planning, Budgeting and Reporting System” (PlanRep) na ule wa usimamizi wa Fedha za Serikali katika ngazi za Msingi zinazotoa huduma za Elimu na Afya “Facility Financial Accounting and Reporting System”.

Kwa namna ya kipekee napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wataalam wote waliohusika kubuni wazo hili, kuliandikia andiko na kuweza kupata ufadhili nje ya Fedha za Serikali, naamini mtakubaliana nami kwamba kazi iliyofanywa na Wataalam wetu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Watendaji wa Mradi wa PS3 inastahili pongezi kubwa.

 

Aidha, napenda kuwapongeza Mradi wa PS3 kwa kuwezesha Mikoa 13 iliyoko kwenye mradi huu kwa kuiwekea miundombinu ya TEHAMA itakayowezesha mifumo hii miwili kuanza kutumika kwenye Idara za Mikoa na Halmashauri za Mradi wa PS3.

 

Vilevile, napenda kuzishukuru Wizara za Kisekta na Taasisi za Serikali kwa michango yao, utaalam na ushauri wao mzuri ambao kwa pamoja umeweza kufanikisha utengenezaji wa mifumo hii bora kwa utendaji kazi wa Halmashauri zetu Nchini. Jambo hili ni kubwa na la kupongezwa kwani limefanywa na wataalam wa Kitanzania na dhana ya matumizi ya “Home Grown Solution - Made in Tanzania” inadhihirika wazi kwa kazi hii.

Ndugu Washiriki

Napenda kutumia fursa hii kutambua mchango mkubwa uliotolewa na Serikali ya Marekani kwa kutoa ufadhili wa utengenezaji wa Mifumo hii, kupitia Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma chini ya Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ninawashukuru sana na tunathamini sana mchango wenu. Tunatarajia ushirikiano wenu zaidi katika miradi na program nyingine zinazofuata zenye maslahi mapana ya Taifa. Naomba pia nitoe shukrani zangu za dhati kwa Viongozi na Watendaji wa Mradi wa Health Promotion System Strengthening chini ya ufadhili wa Serikali ya Uswisi. Sehemu ya ufadhili walioutoa katika utengenezaji wa mfumo wa usimamizi wa fedha za Serikali katika ngazi za msingi za kutolea Huduma ni muhimu sana.

MANUFAA YA MIFUMO YA PLANREP NA FFARS

Ndugu Washiriki,

Ni dhahiri ukamilishwaji wa mifumo hii utasaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa Watumishi hasa eneo la mapokezi na matumizi ya Fedha za Umma. Hii ni kuanzia katika vituo vya kutolea huduma za Elimu na Afya mpaka katika ngazi ya Halmashauri.

Aidha, kwa kuzingatia Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kwa Wananchi (D by D) na kupitia utaratibu wa Serikali Kuu kupeleka Fedha za matumizi ya kawaida na shughuli za maendeleo moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Elimu na Afya, mifumo hii itasaidia kusimamia mapato na matumizi sahihi ya Fedha za Serikali na kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi.

Kama alivyosema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. George Simbachawene, (Mb.) ni jambo la faraja kuona kuwa mifumo hii ambayo imesanifiwa na kuboreshwa kupitia ufadhili wa wenzetu wa PS3, inamilikiwa na kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa Asilimia 100. 

Ni jukumu la wahusika wote kuanzia ngazi za Msingi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kwenye Wizara na Taasisi za Serikali zinazohusika na Mipango, Bajeti na matumizi ya Halmashauri kuhakikisha zinautumia. Mfumo huu ni rafiki, fungamanifu na hautakuwa na matoleo mapya ya mara kwa mara. Vilevile mfumo huu una manufaa makubwa kuwezesha Halmashauri zote Nchini kutoa taarifa zenye uwiano sahihi na kwa urahisi zaidi.

Mifumo hii miwili itaunganisha Idara na Vitengo ndani ya Halmashauri, na kuwezesha Wataalam wanaoandaa taarifa za Uandaaji wa Mipango na Bajeti pamoja na utekelezaji wake wafanye kazi kama Timu moja kwa kuwa mifumo hii imejumuisha matakwa na mahitaji ya sekta zote zilizoko katika Halmashauri zetu. Mifumo itawezesha kupata taarifa sahihi za fedha kuanzia ngazi ya Kituo, Idara mbalimbali, Halmashauri, Mkoa mpaka Wizara za Kisekta na Ofisi ya Rais - TAMISEMI.

WAJIBU, MAELEKEZO NA MAAGIZO

 

Ndugu Washiriki,

Kufuatia kukamilika kwa mifumo hii miwili, sasa ni wajibu wa kila Mkoa, Halmashauri na Vituo vya kutoa huduma za Elimu na Afya kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa mamlaka zinazohusika.

                     

Vilevile, ngazi zote za Mamlaka za Serikali za Mitaa lazima zitoe taarifa za mapato na matumizi kwa Wananchi wanaowahudumia kupitia mikutano, mbao za matangazo, tovuti, vyombo vya habari na njia nyinginezo.

Ndugu Washiriki,

Kuanzia sasa hatutarajii kuona kituo chochote cha kutoa huduma za Elimu na Afya kilichopo chini ya Halmashauri kinakuwa na matumizi yasiyozingatia taratibu na kanuni za fedha za umma au kubadilisha matumizi ya fedha bila kuwasiliana na Mamlaka husika. Matumizi ya fedha yafanyike kutegemea chanzo cha fedha kilichopokelewa kwa wakati na kwa mujibu wa bajeti iliyotengwa kwa mwaka husika.

                                                                        

Ndugu Washiriki       

Mifumo hii imeshirikisha Wizara za Kisekta na Taasisi za Serikali ikiwemo Wakala wa Serikali Mtandao (e-Government Agency-eGA) kuanzia hatua za awali za ukusanyaji wa mahitaji hadi utengenezaji wa mifumo; hivyo basi, mfumo wa uandaaji wa Mipango na Bajeti (PlanRep) pamoja na mfumo wa Usimamizi wa Fedha katika Vituo vya Kutoa Huduma za Elimu na Afya ndio itakayotumika katika Halmashauri na Vituo vya kutolea Huduma za Jamii. Hivyo, iwapo kuna Mdau anataka kushirikiana na Serikali anapaswa kutumia na kuboresha mifumo hii na siyo kuleta mifumo mingine. Uwingi wa mifumo huondoa ufanisi na uwajibikaji.

 

Ndugu Washiriki,

Serikali ina matarajio makubwa na mifumo hii, na nitapenda Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Ofisi yangu zipate taarifa zote za Mipango, bajeti pamoja na taarifa za Fedha zinazopelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa wakati na zikiwa katika ubora wa hali ya juu. Aidha, ni vyema sasa mapungufu na dosari zinazojitokeza wakati wa ufungaji wa Hesabu za Mwisho wa mwaka za Halmashauri ziondoke kupitia mifumo hii.

Ndugu Washiriki

Napenda kutumia fursa hii kuwafahamisha Viongozi na Watendaji pamoja na Wananchi wote kwamba, lengo la matumizi ya mifumo ya TEHAMA ni kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za Serikali na isitumike kukwamisha shughuli au utaratibu wa kazi za Serikali. Hivyo, ni muhimu itumike kwa ufasaha ili kuleta tija inayotarajiwa.

                                          

Kwa kuwa mifumo hii ni ya gharama kubwa kila mmoja wenu kwa nafasi yake ahakikishe anailinda, kuitunza na kuitumia mifumo hii ili iweze kudumu na kuwa endelevu kwa manufaa yetu kama Serikali na faida ambazo tutazipata kutokana na matumizi ya mifumo.

Ndugu Washiriki,

Pamoja na maelezo niliyotoa pia ninaagiza yafuatayo:-

Tovuti za Mikoa na Halmashauri zilizozinduliwa mwezi Machi 2017, ziwe na taarifa sahihi na zinazokidhi mahitaji ya taarifa kwa wananchi na wadau wote. Taarifa za Mipango, Bajeti na Matumizi ya fedha ziwekwe katika tovuti hizo.

 

Kila Halmashauri inapoandaa mipango yake ya mwaka mpya wa fedha wa mwaka 2018/2019 ni lazima kutumia taarifa za mfumo wa mwaka uliopita kufanya maamuzi. Kwa Mikoa na Wizara, taarifa hizi za mifumo zitumike kufanya maamuzi, tathmini na ufuatiliaji.

Mikoa na Halmashauri ianze zoezi la kuboresha miundombinu ikiwemo Mtandao Kiambo (LAN) na kuwa na vifaa vya TEHAMA kama kompyuta pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi wake.

Mikoa na Halmashauri hakikisheni mnasimamia na kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo kwa yeyote atakayebainika kuhujumu mifumo hii ya Serikali.

HALI ILIVYOKUWA KABLA YA MATUMIZI YA MIFUMO

Ndugu Washiriki

Katika taarifa niliyoletewa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI na kwa kuzingatia uzoefu niliopata nikiwa Ofisi ya TAMISEMI, ni kwamba Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kipindi kirefu imekuwa ikitumia gharama kubwa katika kukamilisha zoezi zima la uandaaji wa Mipango na Bajeti. Pia, Halmashauri zimekuwa zikitumia muda mrefu na gharama kubwa kwenye kuandaa na kuwasilisha Bajeti kwenye Mamlaka mbalimbali za Serikali na hata katika ufungaji wa Hesabu.

Hesabu za mwaka 2017/2018 zilizotolewa zinaonyesha kuwa gharama za mchakato wa maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya mwaka kwa Halmashauri 185 ni takriban Shilingi Bilioni 8.32 za kulipia usafiri (Mafuta), posho ya kujikimu, shajala na gharama za kudurufu Vitabu. Gharama hizo hazijumuishi gharama za mawasiliano ya mtandao, Umeme, Simu, matengenezo ya magari na matengenezo ya vifaa vya Ofisi kama vile photocopier, n.k.

Kutokana na gharama hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepata wakati mgumu kwa kujikuta wakitumia fedha nyingi kugharamia maandalizi ya Bajeti na kusababisha Wananchi kukosa huduma kutokana na Wataalam wa Halmashauri kutumia muda mrefu katika mchakato wa zoezi la bajeti. Aidha, maandalizi ya bajeti yamekuwa na changamoto nyingi na kusababisha Halmashauri kuvuka na bajeti kubwa mwisho wa mwaka, kwa kuwa zoezi huchukua muda mrefu. Changamoto hii itaondolewa na matumizi ya mifumo hii.

MWISHO

Ndugu Washiriki

Ni jambo la kutia moyo kwamba, kupitia mfumo huu wa PlanRep changamoto hizi zimetatuliwa na tutaweza kuokoa wastani wa Shilingi Bilioni 4 kila mwaka ambazo ni gharama za Serikali zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya kufanya maandalizi na mchakato wa Bajeti kama kuandaa machapisho, nauli pamoja na posho za kujikimu kwa Watumishi wanaoshiriki kuandaa Bajeti za Halmashauri.

Kabla ya kuhitimisha Hotuba yangu, napenda kuwashukuru Wadau Wetu wa Maendeleo wa USAID na Wadau wengine waliochangia Mradi huu na nawaomba tuendelee kushirikiana katika kuimarisha na kuufanya mfumo huu kutumika kwa ufanisi katika Ofisi zote zinazofanya kazi na Halmashauri. Nitumie fursa hii kuwasilisha, kuishawishi Serikali ya Marekani iweze kuingiza Mikoa 13 iliyobaki ili iweze kujumuishwa kwenye Mradi wa PS3. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wenu na tunaamini kuwa nyie ni wadau wa kweli na kudumu katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya haraka katika Nchi ya Tanzania. Tunawashukuru sana.

 

Baada ya maelezo hayo, sasa nipo tayari kuzindua rasmi Mifumo miwili mipya ya kielektroniki ambayo ni mfumo wa Kupanga Mipango, Kuandaa Bajeti na Kutolea taarifa za hatua za Utekelezaji wa Bajeti (PlanRep - Planning, Budgeting and Reporting System) pamoja na mfumo wa Kufanya Malipo na Kutoa Taarifa za fedha ambazo zimetumwa kwenye Vituo vya Kutoa Huduma (Facility Financial Accounting and Reporting System).

Asanteni Sana kwa Kunisikiliza.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.