Milioni 28 Kukamilisha Ujenzi wa Bweni -Matemanga.
Kufuatia umbali kutoka shuleni hadi nyumbani Halmashauri ya wilaya ya Tunduru katika mwaka wa fedha 2016/2017 imefanikiwa kujenga hosteli yenye thamani ya shilingi milioni 28,000,000.00 kutoka katika ruzuku ya Miradi ya maendeleo (LGCDG) katika shule ya sekondari Matemanga wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma ikiwa ni mkakati wa kupunguza kero ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.
Kukamilika kwa ujenzi wa hosteli katika shule ya sekondari matemanga kutasaidia sana kupunguza kero kwa wanafunzi wanaosafiri umbali mrefu kufuata huduma ya elimu na kwa kupunguza gharama kwa wazazi kwani kwa asilimia kubwa wanafunzi walikuwa wanaishi katika nyumba za kupanga.
“wanafunzi kuishi katika mazingira ya shule kutapunguza usumbufu waliokuwa wanapata wazazi kwa kuwapangishia watoto nyumba mtaani hali ambayo inaleta usumbufu kwa walimu na wazazi”alisema mkuu wa shule ya sekondari matemanga.
Wanafunzi kuishi katika mazingira ya shule itasaidia katika masuala mengi ikiwa ni pamoja na kuweza kudhibiti nidhamu za wanafunzi kwani muda mwingi watukuwa chini ya uangali wa walimu ukilinganisha na awali walipokuwa wanapanga mitaani.
Katika mpango wa bajeti wa mwaka 2016/2017 Halmashauri ilitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli na ukarabati katika shule za sekondari za Semeni, Mataka, Lukumbule, Nalasi, Ligoma na Matemanga Sekondari ikiwa pia miongoni mwa shule hizo.
Uboreshaji wa miundombinu ni miongoni mwa mikakakti ya halmashauri katika kuongeza kiwango cha elimu na ufaulu kwa kuwajengea mazingira Rafiki na wezeshi wanafunzi ili waweze kutumia muda mwingi wa kujisomea.
Serikali itaendelea kuweka katika mpango wa bajeti ujenzi wa hosteli na uboreshaji miundombinu ya shule ikiwa ni pamoja na madarasa, nyumba za walimu na ujenzi wa matundu ya vyoo ili kuweka mazingira Rafiki ya kufundishia na kusomea kwa wanafunzi na kuongeza kiwango cha ufaula katika shule zote kutokana na mazingira ya shule za kata nyingi kuwa mbali na vijiji wanapotoka wanafunzi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.