• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

HALMASHAURI zote nchini zatakiwa kusimamia mapato

Imewekwa : September 27th, 2018


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa (MB) ametoa rai kwa Madiwani, Wakurugenzi na Makatibu Tawala wa Mikoa  kubadilisha mtazamo  katika suala zima  la usimamizi, ukusanyaji na  utumiaji  wa fedha  zinazokusanywa kwenye Halmashauri zote nchini

Akifungua Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika leo katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma. Mhe. Majaliwa amesema ustawi wa jamii unategemea uwezo wa mapato yake na matumizi yenye tija kwa fedha zinazokusanywa

Mhe. Majaliwa amefafanua kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha Halmashauri zinakuwa na uwezo wa kujitegemea kimapato kwa zaidi ya asilimia 80 ifikapo mwaka 2025 ili kutimiza lengo la Serikali katika Dira ya Maendeleo ya 2025.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano imekuwa ikichukua  hatua mbalimbali  ili kuhakikisha dira ya maendeleo ya mwaka 2025 kwa kuanzisha  utaratibu wa kugharamia  miradi  ya kimkakati  yenye lengo  la kuziongezea Halmashauri mapato  ya uhakika  na kupunguza utegemezi  wa ruzuku  ya Serikali.

Mhe. Majaliwa amesema kuwa  hadi sasa Serikali  imeidhinisha shilingi bilioni 131.5 kutekeleza miradi ya  ipatayo 22 katika Halmashauri  17 zilizokidhi vigezo kwenye Mikoa 10 na mpaka sasa kiasi cha shilingi bilioni 16.4 zimepelekwa kwenye Halmasahauri  hizo kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa  miradi ya kimkakati.

Amaesema kuwa  uchambuzi wa miradi  mingine ya kimaendeleo  unaendelea na Halmashauri  zitakazokidhi vigezo zitapata fedha kwa  ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo na amezitaka Halmashauri zote nchini  kutumia fedha  hizo kwa ajili ya  malengo yaliyokusudiwa.

“ Serikali  haitakuwa  na utaratibu wa kutoa fedha bila kufahamu kwa kina fedha hizo zinakwenda kufanya nini na zinaleta mabadiliko gani kwa kuwa nimesikia kwamba katika baadhi ya Halmashauri fedha zilizokwishatolewa bado hazijaanza kutumika kikamilifu, nawaagiza Waheshimiwa Madiwani kusimamia matumizi ya fedha hizo ili Halmashauri  zipate miradi yenye ubora unaotakiwa na inayokamilika kwa wakati” Anafafanua Majaliwa.

Mhe. Majaliwa amesema Serikali imeongeza ukusanyaji wa mapato  katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuhakikisha Halmashauri zote 185 zinatumia Mfumo wa ukusanyaji wa mapato wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na kufanya ongezeko la mapato kutoka shilingi bilioni 379 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia  shilingi bilioni 553.39 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 .

Amewaonya Viongozi wa Halmashauri wanaolalamikia kutokuendelea kulalamika  kuhusu baadhi ya vyanzo  vya mapato  kuchukuliwa na Serikli  kuu bali  waongeze  bidii  na ubunifu  katika kutafuta  vyanzo vipya vya  mapato ili Mamlaka za Serikali za Mitaa  ziweze kujitegemea.

“Fanyeni kazi  ionekane, tusione Mamlaka  za Serikali za Mitaa ambazo kweli zinatoa huduma, tuone vyumba vya madarasa vinaongezeka, watoto hawakai chini, Zahanati zinazopendeza  hapo tunaweza  kusema sasa  Halmashauri zimekomaa” Amefafanua Mhe. Majaliwa

 Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakurungenzi wa Halmashauri kuacha kufanyakazi kwa mazoea bali wafanye kazi kwa bidii kwa kutumia weledi ili  kuleta mabadiliko katika utendaji kazi katika Halmashauri

Aidha Mhe. Jafo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanawake, vijana  na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kiuchumi  na kupunguza umaskini  nchini.

Imetolewa na tovuti ya TAMISEMI

Septemba 27,2018

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.