Mbunge wa Tunduru kaskazini Hassan zidadu kungu alizungumza katika hafla hii ya kumuenzi aliyekuwa Raisi wa kwanza wa Tanzania ,baba yetu wa taifa hayati Mwal. Julius kambarage nyerere, hafla iliyofanyika katika sekondari ya wasichana masonya iliyopo tunduru mjini katika kijiji cha masonya. MH mbunge Hassan kungu alizungumza na vijana hao wa shule hiyo na kuwasisitizia kujitahidi katika masomo yao ya shule ili waweze kufanikiwa katika maisha yao ya baadae , na kuwataka kuepuka vishawishi ambavyo wanakumbana navyo katika jamii zetu ili waweze kutimiza malengo yao waliokuwa nayo.
Katika hafla hiyo pia mgeni rasmi kaimu katibu tawala wawiliaya ya Tunduru ndg. Joshua john aliemwakilisha mkuu wa wiliaya ndg Julius mtatiro katika hafla ya sikukuu ya vijana iliyoambatana na kumbukizi za aliekuwa raisi wa kwanza wa Tanzania Mwal Julius kambarage nyerere , hafla iliyofanyika katika shule ya wasichana masonya wilyani Tunduru . Mgeni rasmi aliwasihii vijana kufata falsa za hayati Mwal Julius kambarage nyerere ,pia alizungumza na vijana juu ya kupigana na maadui watatu ambao baba wa taifa alikuwa akipambana nao ambao ni ujinga ,maradhi na umaskini .
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.