Haya yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh. Juma Z.Homera katika kikao cha tathimini ya Elimu wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa klasta ya mlingoti Tunduru Mjini, ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kiwiliya ya kuinua kiwango cha ufaulu Tunduru.
Akifungua kikao cha tathminiya elimu Wilayani Tunduru kilichohudhuriwa na wadau wa elimu kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Tunduru Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera alisema kwamba katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017 Halmashauri ya Tunduru imeshika nafasi ya tano kati ya Halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma na katika nafasi za kitaifa wilaya ya Tunduru ni ya 179 kati ya Halmashauri 185.
Mkuu wa wilaya Juma Homera aliendelea kusema kuwa ili kuboresha kiwango cha ufaulu katika wilaya ya tunduru idara ya elimu msingi na sekundari iandae mitihani kwa kidato cha nne , pili na darasa la saba kila baada ya miezi 3 ili kuwapima wananfunzi kila mara na kuwajengea uwezo.
Pia alitoa maagizo kwa watendaji kata, vijiji na Maafisa Elimu Kata kufuatilia idadi ya wanafunzi waliojiandikisha darasa la kwanza na awali ambao bado hawajaripoti shuleni na wale wa sekondari wasioripoti shuleni mpaka sasa ili wazazi au walezi kuchukuliwa hatua.
Mwenyekiti wa huduma za jamii ambaye pia ni diwani wa Kata ya Ligoma Mh. Abasi Ngajime akitoa mchango wa kuberesha mazingira ya watoto ambao wazazi wao wanaenda kufanya shughuli za kilimo mbali na mazingira ya kijiji ili weweze kuapata fursa na haki kupata elimu kwani ni haki yao.
“Watendaji wa Kata, Vijiji na Maafisa Elimu kata fuatilieni taarifa za kuandikisha wanafunzi wa awali na darasa la kwanza na watoto wote wenye umri wa kuanzia miaka 4-5 waende shule na mfanye kazi kwa nafasi zenu kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma na msisubiri kusukumwa” alisema Juma Homera.
Afisa Elimu anayeshughulikia wanafunzi wenye mahitaji maalum mwalimu Albart akipokea maagizo kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya kuandaa mahitaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum ili serikali iwezeshe ununuzi wake kupitia mfuko wa Elimu Tunduru.
Aidha akitoa ufafanuzi wa upungufu mkubwa wa miundombinu ya shule katika Halmashauri ya wilaya Tunduru, mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa katika msimu wa korosho wa mwaka 2017/2018 serikali ilianzisha mfuko wa kuchangia elimu na kukata wakulima wa zao la korosho katika kila kilo moja ya korosho sh 30 na zaiadi ya milioni 600 zimekusanywa.
“Niwaombe walimu mtuandalie vipaumbele vya mahitaji ya upungufu wa miundombinu ikiwa ni pamoja na nyumba za watumishi, matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.” alisema Juma Homera
wadau wa elimu wilaya ya Tunduru wakifuatilia kikao cha tathmini ya elimu wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Klasta ya Mlingoti
Na kwa upande wa wadau wa elimu wilayani Tunduru walishauri kwa pamoja mambo yafuatayo yakifanyika kiwango cha elimu kitaongezeka na kufikia malengo ya kuondoa daraja sifuri kabisa.
Kuanzishwa kwa klabu za midahalo (debates), michezo na makongamano ya wanafunzi kati ya shule na shule ili wanafunzi kuweza kubadilishana uzoefu na pia katika kila shule kuwa na majaribio ya mara kwa mara, pamoja na morning speeches, vitu ambavyo vitawajengea uwezo wa kujiami wanafunzi na kujifunzi lugha ya kiingereza.
Afisa Taaluma akisoma taarifa ya Elimu Taaluma Mwalimu Mussa Chandu katika kikao cha Tathimini ya Elimu Wilaya.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.