• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

ELIMU KIPAUMBELE WATOTO WA KIKE

Imewekwa : April 27th, 2017

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mh Mbwana Mkwanda Sudi katika mahafali ya pili ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana Masonya yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo mapema wiki,shule ya sekondari Masonya ilianzishwa mwaka 1994 chini jumuiya ya wazazi na mwaka 2014 shule ilianza kupokea wananfunzi wa kidato cha tano kwa michepuo ya GHL na HGK na kwa mwaka 2017 ina jumla ya wahitimu wapatao 39 ambao 19 ni mchepuo wa HGK na 20 ni HGL.

   Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Mh Mbwana Mkwanda Sudi  wakati wa sherehe za mahafali mkuu wa Shule ya wasichana Masonya Bi Elice Banda alisema shule ya wasichana masonya katika matokeo ya mwaka 2016 ilishika nafasi ya kwanza kimkoa, hivyo ni vyema wahitimu kuongeza bidii na kuhakikisha historia nzuri inaendelea.

Elice Banda alisema pamoja na mafanikio waliyopata katika taaluma bado wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa walimu hasa wa masomo ya sanyansi na baadhi ya masomo ya sanaaa, pia shule ina miradi mbali mbali inayoendeshwa kwa ushirikiano wa walimu na wanafunzi katika dhana ya elimu ya kujitegemea na kujifunza stadi za maisha lakini pia kuongeza kipato cha shule na kumudu kulipa gharama za watumishi wa ajira za muda.

 Akitoa hotuba kwa wahitimu , walezi, wazazi na wanafunzi wa shule ya wasichana masonya mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya kidato cha  Mh Mbwana Mkwanda Sudi ambaye pia ni mwenyekiti wa halmasahuri ya wilaya ya tunduru alianza kwa kushukuru uongozi wa shule , na wahitiumu kwa uvumilivu mkuu walionesha kwa kipindi chote cha masomo bila ya kukata tamaa.

Mh Mkwanda Sudi aliendelea kusema amekisikia kilio cha wanamasonya na serikali imepanga fedha za kutosha katika Bajeti za  Halmashauri ili kuhakikisha wananboresha shule hiyo na kuboresha mazingira ya kusomea kwani inatambua umuhimu mkubwa wa shule na ina mchango mkubwa sana katika jamii.

  Aidha aliendelea kawahusia wahitimu kuyashiki mafunzo yote walijifunza na kwenda kuyaishi na sio wanaenda kuwa mizigo kwa wazazi na jamii na wasikubali kumezwa na malimwengu kwani safari yao y aelimu bado inaendelea,


  Mh mwanda Sudi alisema kuwa elimu ni bahari haina mwisho na kuwataka wahitimu kufikiria kusonga mbele zaidi katika elimu ya juu, na miongoni mwenu ndipo watatoka viongozi mbali mblali wa nchi yetu na sera ya serikali ya uchumi wa kati ifikapo 2015 itafanikiwa kwa asilimia kubwa kwa kuwekeza katika Elimu.

"Elimu ni msingi wa maisha msidanganyike na ya dunia, wananume wasiwadanganye muache kusoma mkaolewe, au wazazi wasiwe sababu ya kushindwa kufikia ndoto zenu,mtakuja kujuta baadaye" alisema Mh Mkwanda Sudi.

  Hata hivyo wanafunzi wa kidato cha tano katika Igizo waliwakumbusha wazazi juu ya haki ya mtoto wa kike kupata elimu ni sawa na mtoto wa kiume na jamii ambazo hawamdhamini mtoto wa kike waone kuwa watoto wote ni sawa na wanastahili kupata haki sawa bila ya kujali jinsi zao, 

 Na wahitimu kutodanganyika ya duniani na kuona mwisho wa kusoma umefika wakati bado kuna safari nje ya darasani na kuna elimu baada ya kidato cha sita, ni wakati wa mtoto wa kike kuamka na kupata haki sawa na mtoto wa kiume.








Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • HARAMBEE YA UJENZI WA OFISI YA CCM TUNDURU YAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 106 PAMOJA NA MIFUKO 15 YA SARUJI.

    December 29, 2025
  • MHESHIMIWA SEFU HASSAN DAUDA NDIYE MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU

    December 05, 2025
  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.