Akisoma taarifa ya mgawanyo wa vifaa vya ujenzi kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru ndg Chiza Cyprian Marando amesema kuwa halmashauri ilianzisha mkakati wa kuondoa changamoto ya miundombinu ya shule kwa kila kijiji kuwa na benki tofali laki moja (100,000) katika mwaka wa fedha 2016/2017, ili kuhakikisha sera ya elimu bila malipo inafanikiwa kwa kuwashirikisha wadau wa elimu.
Katika kutekeleza kauili mbiu ya "Elimu bila malipo, mtoto aende shule kila mdau awajibike" halmashauri ya Tunduru ilianza kwa kuwashirikisha wadau wa elimu katika msimu wa zao la korosho mwaka 2017/2018 kwa kuanzisha mfuko wa elimu, ambapo kwa hiari ya wakulima wa Tunduru walikatwa shilingi 30 kwa kila kilo moja ya korosho.
Fedha hizi zilipelekwa moja kwa moja katika kuboresha miundombinu ya shule na jumla shilingi milioni 608,248,680.00 zilikusanywa “tumefanikiwa kununua malighafi za ujenzi kutoka viwandani kwa bei ya jumla ili kupunguza gharama, vifaa vyenye thamani ya milioni 225,251,040 ambayo ni saruji mifuko8720,bati 3132, na nondo 880 na kuokoa shilingi milioni 36,516,000 ambazo zinaweza kujenga hosteli moja na kukamilika” alisema mkurugnzi mtendaji halmashauri ya Tunduru ndg Chiza Marando.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme akitaka utepe katika uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya ujenzi (aliyevaa Blauzi ya Blue) uliofanyika Nakayaya katika ghala la kuongeza thamani zao la mchele terehe 06/05/2018
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tunduru mh juma zuberi homera wilaya ya Tunduru ina shule za msingi 150, ikiwa 149 ni za serikali na moja ya mtu binafsi na shule za sekondari 23 ikiwa 21 ni za serikali na 2 ni za watu binafsi.
Pia alisema halmashauri ya wilaya ya Tunduru ilikuwa na changamato kubwa ya miundombinu ya elimu, na kufikia hatua ya kupanga mikakati na wadau zao la korosho kuwakata wakulima shilingi 30 kwa kila kilo ya korosho ili kuweza kujenga miundombinu ya shule na kuhakikisha kuwa madarasa ya nyasi wilayani Tunduru yanakwisha.
mkuu wa mkoa wa Ruvuma bi. Christina Mndeme akifuatilia taarifa ya uzinduzi wa mgawango wa vifaa vya ujenzi na Elimu wilayani Tunduru iliyokuwa inasomwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru ndg Chiza Marando.
Akihutubia wananchi na watendaji waliohudhuria katika uzinduzi wa kugawa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya elimu vyenye thamani ya shilingi milioni 225,251,040 mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme aliwataka watendaji kuziogopa fedha hizo za elimu kama kimeta kwani watafuatilia na kufanya ukaguzi wa namna zitakavyotumika.
Aliendelea kutanabaisha kwa Maafisa elimu Kata, wakuu wa shule na Walimu wakuu, watendaji wa Kata na waheshimiwa madiwani, bodi za shule na kamati za ujenzi za shule kufanya usimamizi wa kila siku ili kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa malengo kusudiwa.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme (wa tatu kutoka kushoto) akiwapongeza viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru kwa ubunifu wa kutatua changamoto za elimu, baada ya kufaya zoezi la uzinduzi la ugawaji wa vifaa vya ujenzi vyeneye thamani ya shilingi milioni 225,251,040 wa wakuu wa shule za mchangani, umoja ambao waliwakilisha shule zingine zenye mradi wa ujenzi kupitia fedha za mfuko wa elimu wa zao la korosho mwaka 2017/2018.
Aidha Bi Mndeme alisema aliagiza kwa shule ambazo wamepelekewa miradi hiyo kuwa anatoa muda wa miezi mitatu ili kuhakikisha kuwa ujenzi umekamilika. “ninaomba shule zote zilizopokea miradi kuhakikisha kuwa ndani ya miezi mitatu ujenzi umekalimika, kama ni darasa, nyumba ya mwalimu, hosteli au matundu ya vyoo view vimekamilika ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kusomea kwa wanafunzi”
Hata hivyo mkuu wa mkoa aliwataka watendaji kuwa waaminifu na kufanya kazi ya usimamizi kwa weledi na kuepuka tamaa na kuhakikisha kuwa vifaa hivyo inasafirishwa na kufikishwa katika shule bila ya ubabaifu na kuepukana na udanganyifu kwani serikali haitosita kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.