Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndugu Gasper Zahoro Balyomi leo tarehe 13/06/2021 amemkabidhi mganga mfawidhi wa kituo cha Afya cha Nalasi uku akimpatia maelekezo ya kutunza gari hilo maana huduma mbalimbali zinaweza tolewa endapo mgonjwa atakuwa ndani ya gari hilo.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amewataka wananchi kuonesha ushirikiano katika utuzaji wa gari hilo la kubebea wagonjwa katika tarafa ya Nalasi uku akiwataka Wananchi wa tarafa hiyo ya Nalasi wajitaidi kukata bima ya Afya iliyoboreshwa kwa kiasi cha elf 30 tu katika kaya ambayo itahudumia watu sita (6) katika kaya husika.
Pia Mkurugenzi Mtendaji amewambia Wananchi wa Tarafa ya Nalasi kuwa hizo fedha watakazo lipia bima ya afya iliyoboreshwa ndizo pesa zitakazo tumika kulitunza gari hilo ambalo limekuwa mkombozi mkubwa kwa Wananchi wa Tarafa ya Nalasi .
Mwisho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru amemshukuru sana Mheshimiwa Mbunge wa Tunduru kusini Ndg Daimu Idd Mpakate kwa juhudi zake za kuhakikisha anapambana kumuomba Mheshimiwa Waziri mkuu Ndg Kassim Majaliwa Majaliwa hilo gari la Wagonjwa ambalo leo Wananchi wa Tarafa ya Nalasi Wamekabidhiwa.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.