Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh Juma Zuberi Homera katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yenye kauli ya Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu, katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya baraza la Idd wilayani Tunduru .
Mh.Homera ameitaka jamii kutoa na ushirikiano na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na unyanyasaji wa wanawake na watoto unaofanywa katika familia, ikiwa ni pamoja na wanaume kuwalawiti watoto wa kuwalea, masuala ya mirathi na maendeleo katika familia.
Alisema "imekuwa ni kawaida kwa wanaume wengi kutumia mabavu hasa pale wanaposhauri na wake zao masuala ya maendeleo, na badala yake huwakatili wake zao kuamua kuongeza au kuoa mke mwingine, ili kuepuka hayo wanawake wengi wananyamaza kimya ili kulinda ndoa na kushindwa kudai haki zao dawati la jinsi polisi liko wazi"
Mkuu wa wilaya alisema kumekuwa na tabia ya wananchi kutotoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa taarifa za wahalifu waliopo katika maeneo yao, akitoa mfano wa mkazi mmoja wa Kata ya Majengo wilayani Tunduru aliyekuwa anajihusisha na biashara haramu ya kusafirisha wanafunzi wa sekondari kuwapeleka katika nchi jirani kufanya kazi za ndani na uchimabji wa madini, hali wazazi wanakaa kimya bila ya kutoa taarifa kwa vyombo husika.
"niwatake waalimu wote kufanya ufuatiliaji wa wanafunzi katika mahudhurio shuleni ili kubaini na kudhibiti utoro na kama ukiona mwanafunzi hajahudhuria shule zaidi ya wiki basi chukua hatua za makusudi, ufuatiliaji uanze mara moja ili kunusuru mabinti wetu wanajiingiza katika mambo yanayokatisha ndoto zao" alisema mkuu wa wilaya ya Tunduru.
wanawake wakiwa katika maandamano kueelekea katika uwanja wa baraza la Idd ambapo maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kiwilaya yamefanyika
Serikali imeboresha sekta ya elimu wilayani Tunduru kwa kuanzisha shule ya kidato cha kwanza hadi sita ya masonya sekondari na nandembo sekondari kidato cha tano na sita lakini pia kuna mikakati ya kuanzisha shule nyingine za wasichana ili kuwanusuru watoto wanaokatisha masomo kutokana na kupata mimba mashuleni.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Tunduru mh.mbwana mkwanda sudi ambaye pia ni diwani wa kata ya Mchoteka aliwaomba wazazi kutoa mkazo katika elimu ya watoto wao hasa wa kike.
Aidha aliwaasa wanawake kuacha kubagua na kuchagua baadhi ya kazi na kusema hizi ni kazi za wanaume, pia kufanya marejesho ya mikopo ili asimilia 10 ya mapato ya ndani inayotengwa na halmashauri iwanufaishe wanawake wengi zaidi na kupunguza umaskini.
Akitoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto mwakilishi wa dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi Tunduru ndg Tumaini Msowoya alitoa ombi kwa walimu kuwa marafiki wa wanafunzi badala ya kutumia viboko kama sehemu ya adhabu tuu pale mwanafunzi anachelewa shule au kuwa mtoro, kwani kufanya hivyo kutajenga urafiki na wanafunzi hivyo kujua changamoto nyingizinazowakabili.
Takwimu za kiwilaya zinaonesha mimba za utotoni kwa kipindi cha mwaka 2018 pekee jumla ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 3277 wamejifungua katika hospitali ya wilaya ya Tunduru, kati yao 38 walipoteza maisha na 50 kujifungua kwa upasuaji.
katika picha ni wanawake wajasiamali wa wilaya ya Tunduru wakimsikiliza mgeni rasmi ambaye hayuko katika picha wakati akitoa hotuba kwenye maadhimishi ya siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika viwanja vya bazara la Idd Tunduru.
"hali hii ni mbaya sana kwa wilaya yetu kwani changamoto ya wafanyakazi na viongozi wanawake itaongezeka kwani ni kundi kubwa sana la watoto wanaacha kufikia malengo na ndoto zao, wazazi fanyeni majukumu yenu mnapoenda mashambani kulima muwaachieni watoto wenu vyakula ili wasiingie kwenye vishawishi vya mimba za utotoni"alisema bi mwageni.
Hata hivyo maadhimisho hayo yalipambwa kwa bidhaa mbalimbali kutoka katika vikundi vya wajasiriamali wanawake ndani ya wilaya ya Tunduru, naye mgeni rasmi pamoja na wageni wote walipata fursa ya kuona kazi zinazofanywa na vikundi vinavyowezeshw ana halmashauri ya Tunduru, huku wakioomba kuletewa wakufunzi wa kutoa mafunzo ya ili kuongeza kasi ya uzalishaji.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.